ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 6, 2015

BREAKING NEWS IBRAHIMU LIPUMBA AJIUZULU UENYEKITI CUF

Ibrahim Lipumba

Habari zlizotufikia hivi sasa zinasema mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba ameamua kujiuzulu wadhifa wake wa mwenyekiti katika chama hicho.

Vuguvugu za kujiuzulu kwake zilianza juzi katika mitandao ya kijamii baada ya mwenyekiti huyo kutoonekana kwenye mkutano mkuu wa UKAWA walipompitisha Edward Lowassa kupeperusha bendera ya UKAWA kwenye mbio za Urais 2015 na Juma Dudi Haji kama mgombea mwenza.

Vijimambo inaendelea kulifuatilia swala hili kwa karibu zaidi stay tuned.

5 comments:

James Bond said...

Hongera Dr.kwa kutambua alama za nyakati. .nguvu mpya ari mpya vinahitajika ..uenyekiti usiokuwa na mwisho siyo demokrasia! ! UKAWA ndiyo msiba wa CCM. ...Lowassa ndiyo tumaini letu ktk kutokome udhalimu wa CCM.

Unknown said...

Ni huzuni kuona Prof. Anajiuzulu akini mapenzi yake yatimizwe ila ajue kuwa tumesikitishwa na uamuzi wake

Anonymous said...

James bond upon ukawa then unampongeza lipumba dah james. Baba

Anonymous said...

Dalili za mvua ni mawingu. Mawingu ya mporomoko wa Ukawa yameanza na yanaendelea kujitokeza kwa kishindo kikubwa. Viongozi wawili waliokuwa na madaraka makubwa sasa wameaga. Ingawa diplomasia inatumika katika kuaga kwao (ati mmoja amepewa likizo na mwingine sasa atafanya kazi ya utafiti zaidi), ukweli ni kuwa viongozi hao sasa wametoa talaka katika ndoa yao kufaana na Ukawa. Tatizo ambalo upinzani itabidi kujifunza ni kuwa pale mwenzako anaposhindwa kumthitibiti wewe utakuwa na uwezo gani wa kumsimamia na kumfanya aheshimu wajibu wake. Huyo bwana mliyempokea ameshindwa kuelewa kwa nini kaenguliwa na wenzake huko alikotoka na nynyi bila kukaa naye kwa muda na kumuelewa lengo lake ni nini katika ujio wake kwenu mnampokea bila masharti na mara mnampa wadhifa wa kuwa mgombea pekee katika nafasi ya urais. Hamuoni kama hilo ni tatizo na ndilo linaleteleza uhamaji wa viongozi wenu mahili na walioheshimiwa na wanachama kwa muda mrefu? Hakika kama hali itaendelea kuwa hivyo basi itakuwa sawa mtu akisema kuwa upinzani nchini uko katika kinyang'anyilo cha kutoweka.

Anonymous said...

Well stated, mdau wa hapo juu @11:30 AM. Wenzetu wazungu wanaiita hii kama "Marriage of convenience", and in most cases such marriages don't last. Haitapita miezi baada ya uchaguzi, ukawa itakuwa kwenye archives.