Tuesday, August 18, 2015

UZINDUZI WA MRADI WA MAJI NA KITUO CHA MAENDELEO YA VIJANA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Bavuai Migombani Mkoa wa Magharibi Unguja leo alipofika kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua Mfereji, (Bomba la maji), ikiwa ni ishara ya kuzindua Mradi wa maji safi na Salama wa Jimbo la Kikwajuni leo katika viwanja vya Mnara wa Mbao Kilimani Wilaya ya Magharibi A Unguja (katikati) Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Hamad Yusuf Masauni,
Dkt. Shein akimtwisha ndoo ya maji mkazi huyu wa Unguja, baada ya kuzindua Mradi huo wa maji
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo wakati alipotembelea mabanda ya maeonesho ya kazi mbali mbali katika kituo cha Maendeleo ya Vijana Mwembe madema leo akiwa katika ziara ya kuzindua Mradi wa Maji na Kituo hicho katika Jimbo la Kikwajuni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) Nd,Abdalla Suleiman (kulia)wakati alipotembelea kituo hicho Mwembe Madema kuona maendeleoya kazi mbali mbali zinazofanywa na vijana wa Jimbo la Kikwajuni sambamba na uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na Salama katika Jimbo hilo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa Maji safi na Kituo cha maendeleo ya Vijana (Tanzania Youth ICON) huko Mwembe madema Jimbo la Kikwajuni

1 comment:

Anonymous said...

Na ufike wakati tena. Hizi zama za viongozi wa kiafrika kuacha kazi wakenda kufungua visima na barabara tuachane nayo. Mambo haya yafanywe na masheha wa maeneo husika tu. Viongozi wetu wakuu wakae na kutafakari mambo makubwa ya kuleta mabadiliko ya kwa juu Zaidi. Mfano kujenga Hospitali za kina mama na watoto. Kufikiria namna kupambana na tatizo sugu la ajira kwa vijana na kuboresha maisha ya wazee wasio na kazi kwa kuwapatia mafao ya kujikimu.