ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 17, 2015

NEC YATANGAZA VITI VYA MADIWANI WATEULE 1393

              Mkurugenzi wa Uchaguzi wa  NEC Bw. Kailima Ramadhani                           akizugumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya  viti maalumu vya Udiwani ambavyo Madiwani wake wameteuliwa na Tume hiyo  ni viti 1393, kutoka katika Vyama vya CCM,CHADEMA,NSSR-MAGEUZI pamoja na CUF.Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam ,Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Sheria wa NEC Emmanuel Kawishe.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uchaguzi wa  NEC Bw. Kailima Ramadhani.(Picha na Emmanuel Massaka )


TUME ya Taifa ya Uchaguzi( NEC) imesema hadi sasa viti maalumu vya Udiwani ambavyo Madiwani wake wameteuliwa na Tume hiyo  ni viti 1393, kutoka katika Vyama vya CCM, CHADEMA, NSSR- MAGEUZI  pamoja na CUF.

Hayo yamesemwa leo Jijijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati akitoa  taarifa kwa Umma kuhusu uteuzi wa madiwani wanawake wa Viti Maalumu.

Aidha Bw.Ramadhani amesema kuwa idadi ya Viti maalumu Vya Udiwani ni  1,408 nakwamba kutokana na majimbo nane na kata thelathini na Nne ambapo  Uchaguzi haujakamilika kwa Sababu mbalimbali, hatua hiyo itasababisha kubakia viti 15 ambavyo vitagawanywa mara baada ya Uchaguzi kukamilika ili kufikia idadi ya viti 1,408 kutoka viti 1393 vinavyo tambulika kwa sasa.

Aidha amefafanua kuwa kutokana na Viti hivyo  Maalumu Vya Udiwani Vilivyoteuliwa  na NEC, Chama Cha Mapinduzi CCM kimepata viti 1,022,Chama Cha Demokrasia na Mawendeleo CHADEMA 280,Chama Cha Wananchi CUF-79, ACT WAZALENDO viti 6 pamoja na NSSR  MAGEUZI viti 6.

Amesema kuwa tume imeamua kutoa taarifa ya uteuzi wa  viti maalumu Vya Udiwani Nchi nzima ya Madiwani waliyoteuliwa na Tume  kutokana na Kanuni za Kudumu za Mikutano ya Halmashauri, Mabaraza ya Madiwani yanatakiwa kuitishwa siku thelathini tangu tarehe ya Uchaguzi ifanyike.

Katika hatua Nyingine Mkurugenzi huyo wa Uchaguzi  NEC amesema kuwa  mwisho wa Uchaguzi katika Majimbo na Kata ambazo hazikufanya Uchaguzi ni Desemba 20 mwaka huu, ambapo katika jimbo la Uranga Mashariki pamoja na Lushoto uchaguzi utafanyika Novemba 22 mwaka huu,nakuwaomba  Wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuchagua kiongozi wanaomtaka.

2 comments:

Anonymous said...

PALE NIKIKUONA TUU KAILIMA NAPATA PICHA YA MWIZI MKUBWA,ADUI NAMBARI MOJA WA WATANZANIA WALIOWENGI WALIOPIGA KURA TAREHE 25 OCTOBA 2015 JUMAPILI TENA KWA WINGI WA REKODI WEWE KAILIMA,MWENZIO KAPILIMBA JANUARY MAKAMBA NA WALE WAKENYA WA RAILA ODINGA MKALAZIMISHA NA KUYAPINDUA MATOKEO.LAANA ZA WENGI ZITAWAFIKA.SISI TUNAZIDISHA MAOMBI NA DUA ILI HATIMAYE USHUSHWE MKONO WA HAKI,HAKI PEKEE ITATIMILIKA.

Anonymous said...

ewe mwenyezi mungu mtukufu na mwabudiwa wa wote, tunakuomba mola wetu utusikilize kilio chetu cha manyanyaso na mateso dhuruma wizi,ulaghai tuliofanyiwa na wale waliokabidhiwa kwa kiapo dola ya tanzania kwamba watawale kwa kutenda haki,kwamba kwa makusudi yao mabaya hawakutii kiapo chao ambacho walikuhusisha mola wetu kwa kubeba vitabu vitakatifu wakiapa.wameiacha mola wetu,nchi na wananchi wake wa tanzania kwenye majonzi makuu,masononeko,mioyo kukata tamaa.tunakuomba baba,mola wetu mkuu na mtukufu uwape funzo madhalimu hawa ili watambue kwamba madhalimu hutanguliziwa adhabu yao hapa hapa duniani ili waja wako watendewa wawashuhudie,eemin.