Tanzania imeibuka kidedea Jumamosi hii kwenye tuzo za African Magic Viewers Choice Awards 2016 zilizotolewa jijini Lagos, Nigeria.
Kwenye tuzo hizi Elizabeth ‘Lulu’ Michael na Single ‘Richie’ Mtambalike walishinda tuzo moja moja.
Richie ndiye aliyekuwa wa kwanza kushinda tuzo ya filamu ya Kiswahili (Best Indigenous Language Movie/TV Series – Swahili) kwa filamu yake Kitendawili.
“Asante Afrika, asante Tanzania, asanteni wasanii wenzangu kwa kuniunga mkono, asante familia yangu,” alisema Richie wakati akipokea tuzo yake.
“Thank you for calling a spade a spade, not a big spoon, thank you so much,” aliongeza Richie.
“Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru watanzania wote kwa kunisupport katika kazi zangu.Na kwa wote mlionipigia kura nawashukuru mno sina cha kuwalipa zaidi ya kusema Ahsante.Kwa wasanii wenzangu ahsanteni,huu ni mwanzo mpya,” ameandika Richie kwenye Instagram.
Lulu alifuata baadaye na kushinda tuzo ya filamu bora Afrika Mashariki (Best Movie – East Africa) kupitia Mapenzi. Muigizaji huyo alijikuta akilia kwa furaha wakati akishukuru kushinda tuzo hiyo.
No comments:
Post a Comment