ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 14, 2016

MADAKTARI NA WAUGUZI JIJINI ARUSHA WAFIKIWA NA LANCET TANZANIA LTD,YAFUNGUA MAABARA YA KISASA JIJINI ARUSHA

Mtafiti wa magonjwa mbalimbali Dkt Ahmed Kalebi akizungumza na madaktari na wauguzi kutoka katika Hospitali mbalimbali za jijini Arusha,wakati wa warsha iliyofanyika katika jengo ilipo Benki ya ABC.
Baadhi ya Madaktari na wauguzi katika Hospitali mbalimbali za jijini Arusha wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mtafiti wa Magonjwa mbalimbali Dkt Ahmed Kalebi (hayupo pichani)

Mtafiti Dkt Kalebi akizungumza juu ya ugonjwa a kisukari namna ambavyo umekuwa ukiwasumbua watu wengi kwa sasa.
Madaktari na wauguzi wakifuatilia mada.
Dkt Kalebi akisikiliza maswali kutoka madaktari mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu magonjwa mbalimbali 
Mganga Mfawidhi wa Hosptali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru ,Dkt Jackline Urioh akizungumza namna ambavyo watashirikiana na Lancet Tanzania Ltd katika kutumia maabara ya kisasa iliyofunguliwa jijini Arusha kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali.
Mtafiti Dkt Ahmed Kalebi (kulia) akimshukuru mganga mfawidhi Dkt Jackline Urioh mara baada ya kutoa neno kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa katika warsha hiyo iliyoenda sanjari na ufunguzi wa maabara ya kisasa ya Lancet.
Mmoja wa Madaktari waliohudhuria warsha hiyo akiuliza swali .
Washiriki wa warsha hiyo wakifurahia jambo mara baada ya kupata maelezo mbalimbali kuhusu magonjwa ya Saratani na Kisukari.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: