Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imewaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando na mkewe Eva Mhando .
Mhando na wenzake walikuwa wanashitakiwa kwa makosa sita likiwemo la matumizi mabaya ya ofisi, kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Mhando alikuwa anatuhumiwa kwa matumizi
mabaya ya madaraka kwa kuipa zabuni Kampuni ya Santa Clara Supplies
Ltd huku akijua ana maslahi nayo na kwamba anaimiliki yeye, mke na
watoto wake.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwa niaba ya Hakimu mwenye kesi hiyo Kwei Lusema amesema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibisha juu ya matumizi mabaya ya ofisi kwani Mhando alikuwa haingii kwenye vikao vya maamuzi ya bodi ya Tanesco kwa hiyo alikuwa hana ushawishi wa moja kwa moja kushawishi kampuni ya Santa Clara ambayo ni ya mke wake ipatiwe tenda
No comments:
Post a Comment