ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 13, 2016

MHE. JANUARY MAKAMBA AFUNGUA WARSHA YA WADAU WA MAZINGIRA YA NDANI NA NJE YA NCHI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akifungua warsha ya wadau wa Mazingir wa ndani na nje ya Nchi iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais juu ya kujadili jinsi Wafadhili wanavyoweza kusaidia Ofisi katika kuimarisha mambo mbalimbali ya mazingira.
Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo wanaojihusisha na Mazingira hapa Nchini Mh. Egon Kochanke akiongea wakati wa warsha hiyo.
Sehemu ya Wahudhuriaji wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba(hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Luhaga Mpina na kushoto ni Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mh. Egon Kochanke

No comments: