Kwanza kabisa familia ya marehemu inapenda kuwashukuru sana wanajumuiya kwa ushirikiano ambao mmeuonyesha hadi sasa katika kipindi hiki kigumu.
Pili, familia inawashukuru sana wote waliofika kutoa salamu zao za pole kwa njia zote pamoja na rambirambi itakayosaidia kwenye gharama za wasindikizaji. Tunamwomba Mungu azidi kuwabariki na awazidishie pale palipopungua.
Ifuatayo ni update ya tulipofikia mpaka sasa kuhusu usafirishwaji wa mwili wa Marehemu Henry Kiherile
1: Kila kitu kinakwenda vizuri na tunategemea vibali vyote vitapatikana kwenye muda uliopangwa
2: Mwili wa marehemu unategemea kuondoka Jumapili April 17th 2016, kuelekea Dar-es-Salaam Tanzania kwa mapumziko yake ya mwisho siku ya Alhamisi April 21st 2016.
3: Tutakuwa na Misa fupi ya kumuombea na kumuaga marehemu itakayofanyika siku ya Jumamosi April 16th 2016, kuanzia saa nane mchana (2:00 PM) kwenye kanisa la Memorial Drive Lutheran Church kwenye anuani ifuatayo:
12211 Memorial Dr at Gessner Rd Houston, TX 77024.
4: Tutakua na chakula na vinywaji (Soft drinks only Kanisani) Mara baada ya Misa ya marehemu hapo kanisani.
5: Kwa wageni ambao watapenda kwenda nyumbani kwa wafiwa, wanakaribishwa baada ya ibada ya kumuaga marehemu kukamilika katika anuani ifuatayo hapo chini:
8107 Meadows Pond DR, Missouri City, TX 77459
(Vinywaji kama pombe vinaruhusiwa nyumbani kwa wafiwa)
6: Tunawaomba mjitahidi kufika kwa muda uliopangwa.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Kwa niaba ya familia.
Cassius Pambamaji
THC Spokesman
3 comments:
Maskini henry .kwa nini watu wazuri wanakufa kikatili.pole sana ANNA MAKINDA
Ni mtoto wa mdogo wa aliekuwa speaker wa bunge ANAITWA mebo .Nafikiri Annie makinda ndio mlezi.Hata msiba hapa houston upo kwa mdogo wake Annie makinda .Lucy makinda tenende.
Poleni wana makinda kwa msiba mzito .gone too soon henry
Post a Comment