Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maabara za Vetenari Tanzania "TVLA" Dkt. Furaha Mramba akiwakaribisha baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini Oman waliopo nchini kwa ziara ya siku tatu (3) inayomalizika leo, ambao walitembelea katika Taasisi ya utafiti na uchunguzi wa wadudu na magonjwa waenezayo "VVBDRI -TANGA" inayosimamiwa na wakala hiyo na kutembelea sekta ya mifugo ili kuweza kujionea fursa za uwekezaji kupitia miradi hiyo.
Kiongozi wa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Oman Bw. Warith Al- Kharusi akieleza malengo ya ziara yao Mkoani Tanga ambapo alieleza kuwa wamekuja kutembelea mradi wa shamba la mifugo ili waweze kujionea fursa za uwekezaji zinazoweza kupatikana kupitia mradi huo na miradi mingine watakayoitembelea.
Afisa Mambo ya Nje kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Bw. Hangi Mgaka wa pili kutoka kushoto ambaye pia aliratibu Ziara hiyo akifuatilia uwasilishaji wa taarifa kabla ya ziara kuanza.
Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Omani wakiongozwa na viongozi wakuu na maafisa wa Taasisi za TVLA na VVBDRI-TANGA wakiwasili katika shamba la utafiti Mivumoni lililopo Wilayani Pangani Mkoani Tanga lenye ukubwa wa ekari 12789.6 ili kuweza kuona shughuli za ufugaji zinazofanyika katika shamba hilo
Bw. Warith Al - Kharusi akijadili jambo na wafanyabiashara wenzie wakati walipokuwa wakitembelea shamba hilo linalofuga Ngo'mbe, mbuzi na Kondoo, ambapo mpaka sasa Taasisi ya VVBDRI - Tanga imeweza kutumia asilimia 20 ya shamba hilo kwaajili ya shughuli za ufugaji na sehemu inayobaki bado haitumiki.
Dkt. Mramba akielezea utengenezaji wa marobota ya nyasi kwaajili ya malisho ya mifugo na uhifadhi wake unavyofanyika katika shamba hilo, ambapo Wafanyabiashara hao walivutiwa nazo na kuonesha nia ya kuwekeza katika katika uzalishaji huo ili shamba hilo ambalo sehemu kubwa ya eneo lake halijafanyiwa matumizi liweze kuzalisha nyasi hizo kwa wingi kupitia teknolojia za kisasa na kuweza kuwa na tani za kutosha kusafirisha kwaajili ya mauzo nje ya nchi
===================================================
Wakati huo huo wafanyabishara hao pia walitembelea katika kiwanda cha kuzalisha maziwa "TANGA FRESH LTD" kilichopo eneo la Kange Jijini Tanga
Mkuu wa Idara ya Fedha katika kiwanda cha Tanga Fresh BW. Clemence Winfredy akiukaribisha ujumbe wa wafanyabiasha kutoka Oman waliotembelea kiwanda hicho ili kujionea shughuli za uzalishaji
Bw.Clemence Winfredy akiwasilisha taarifa ya shughuli za uzalishaji wa kiwanda pamoja na kuainisha fursa za uwekezaji zinazopatikana katika kiwanda hicho
Sehemu ya wafanyabishara wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ambapo pia waliweza kushauri baadhi ya maboresho kwaajili ya kuongeza uzalishaji na usindikaji wa maziwa
Wafanyabiashara wakitembelea eneo la uzalishaji wa maziwa
Wakiangalia na kupokea maelezo namna uzalishaji wa maziwa unavyofanyika hadi hatua ya kufungasha na kwenda sokoni
Matanki kwaajili ya kuhifadhia maziwa yaliyokwisha kamilisha hatua zote za utayarishaji na kuwa tayari kwa kufungashwa
Ujumbe wa wafanyabiashara ukiondoka mkoani Tanga mara baada ya kukamilisha ziara
No comments:
Post a Comment