ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 25, 2016

Mama wa Mitindo Asya Idarous awa kivutio kikubwa Atlanta GA katika Shikamoo festival

Pichani Asya Idarous akiwa katika tukio hilo la tamasha la Shikamoo Swahili Fest, Atlanta, GA lililofanyika Jumamosi ya Oktoba 22.2016
Mama wa Mitindo anayefanya vizuri ndani ya Tanzania na Nchini Marekani, Asya Idarous Khamsini jumamosi ya Oktoba 22 ameweza kukonga nyoyo za watu mbalimbali waliofika katika tamasha la Shikamoo Swahili Fest, Atlanta, GA lililokuwa maalum kuenzi Kiswahili kama lugha ya Afrika Mashariki pamoja na tamaduni zake ambapo mavazi yake pia yalikuwa kivutio.
Mwanamitindo Asya Idarous Khamsini ameweza kuonyesha mavazi mbalimbali ya asili ya Tanzania na utamaduni wake na kubainisha kuwa mengi ya mavazi hayo, yalikuwa kivutio kikubwa huku vazi la Baibui la kizamani yakiuzwa kwa wingi kutokana na kupendwa na wengi kwenye tukio hilo.
Aidha, mbali na mavazi, pia kulikuwa na mambo mbalimbali ikiwemo michezo ya kitamaduni, vyakula vya asili, huku mijadara na mambo mbalimbali na mambo mengine kibao ikiwemo michezo yhya watoto.

No comments: