Mtandao wa mabadiliko ya tabianchi umetoa tamko lake juu ya Mapendekezo
ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/18 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango
na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 ambao ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa “Mpango
wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21)” wenye dhima ya “Kujenga
Uchumi wa Viwanda ili Kuchochea Mageuzi ya Uchumi na Maendeleo ya Watu”.
Katika taarifa yao pamoja na kutambua kuwa suala la ‘Mabadiliko ya Tabianchi’ limeainishwa kama moja ya maeneo ya kuzingatia kwa ukuaji wa uchumi na ustawi wa taifa, wametoa mapendekezo yako katika maeneo makuu matano.
Kwa kifupi mapendekezo hayo ni pamoja na Mabadiliko ya tabianchi ni suala
la kiuchumi na ni zaidi ya suala la mazingira pekee, Utekelezaji wa miradi ya
maendeleo ikiwemo miundombinu izingatie masuala ya mabadiliko ya tabianchi, Kuongeza
mgawanyo wa matumizi katika miradi ya maendeleo kulinganisha na kawaida, Ufuatiliaji
na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya mabadiliko ya tabianchi na Ushirikishwaji
wa wadau. Soma zaidi
No comments:
Post a Comment