ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 9, 2017

Afa kwa kugongwa na gari baada ya kujirusha barabarani

By Twalad Salum, Mwananchi tsalum@mwananchi.co.tz

Misungwi. Mkazi wa Kijiji cha Igokelo wilayani hapa Mkoa wa Mwanza, Matha Stephano (46) amefariki dunia kwa kugogwa na gari baada ya kujirusha barabarani kwa madai ya ugumu wa maisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jana kuwa Stephano alijirusha barabarani Januari 6, na kugongwa na gari aina ya Scania lililokuwa likisafiri kwenda Dar es Salaam.


Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya hiyo, Robert Mapinda alithibitisha kupokea mwili wa Stephano kutoka Kituo cha Polisi cha Misungwi.

Alisema Stephano alipasuka kichwa na kuvunjika mguu wa kushoto, pia alitokwa damu nyingi.

No comments: