Advertisements

Monday, October 16, 2017

IBADA YA MISA YA KUMWOMBEA MPENDWA WETU JOSEPH NDYAMUKAMA BALTIMORE, MARYLAND

 Zulia lililonakshiwa na picha ya marehemu Joseph Ndyamukama aliyefariki Sept 25, 2017 na siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 kufanyika Ibada ya misa ya kumwombea marehemu katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production.
Picha na kisanduku kilichowekwa majivu ya mpendwa wetu Joseph Ndyamukama kwenye ibada ya misa ya kumwombea marehemu iliyofanyika siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani.

 Padri Honest Munishi akiongoza ibada ya misa ya kumwombea marehemu Joseph Ndyamukama iliyofanyika siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani.
Orgence Matungwa ndugu ya marehemu akiwa na mkewe wakiwasha mishumaa muda mfupi kabla ya kuanza kwa ibada ya misa ya kumwombea marehemu Joseph Ndyamukama iliyofanyika siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani.
Padri Honest Munishi akiongoza ibada ya misa ya kumwombea marehemu Joseph Ndyamukama iliyofanyika siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani.
Familia ya marehemu ikifuatilia ibada.
WanaDMV waliojumuika pamoja kwenye ibada ya misa ya kumwombea marehemu Joseph Ndyamukama iliyofanyika siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

Joseph Mzanila rafiki wa karibu na marehemu akisoma somo la kwanza na baadae mwisho wa misa ya kumwombea marehemu Joseph Ndyamukama alielezea jinsi alivyomfahamu marehemu.
Irene mmoja ya marafiki wa karibu na familia akisoma somo la pili
Padri Honest Munishi akisoma neno la injili
 Padri Honest Munishiakihubiri neno la injili.
Mwambata wa jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Col. Adolph Mutta akitoa salamu kutoka kwa. Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Wilson Masilingi.


Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akielezea jinsi alivyokutana na marehemu nasiku hiyo marehemu aliomba wapige picha ya pamoja na picha hiyo ndiyo iliyokua ikitembea kwenye mitandao kumtambua marehemu mara baada ya kifo chake kutangazwa kwenye mtandao wa Polisi wa Montgomery .
 Orgence Matubgwa akisoma wasifu wa marehemu na salamu kutoka kwa mke wa marehemu ikiwemo barua ya shukurani kutoka kwa familia ya marehemu, Tanzania.
Jessica Mushala akielezea jinsi alivyomjua marehemu napia alikua mtu wa aina gani.
Katibu wa Jumuiya ya wa Katoliki Minja akitoa shukurani zake akiwa pamoja na viongozi wengine wa Jumuiya hiyo ya Katoliki ya misa ya Kiswahili.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Katoliki misa ya Kiswahili PatrickKajale akifafanua jambo nakuwaomba wanaDMVwaliohudhuria ibada ya misa ya kumwombea marehemu Jeseph Ndyamukama utaratibu wa kumchangia ndugu wa marehemu awezekuambatana na majivu ya marehemu kwenda Tanzania kwenye mapunziko ya nyumba yake ya milele.

Mshereheshaji Tuma akiratibu ratiba ya ibada ya misa ya kumwombea marehemu Joseph Ndyamukama iliyofanyika siku ya Jumapili Oktoba 15, 2017 katika kanisa la Mt. Edward Baltimore, Maryland nchini Marekani.
Mark akiwashukuru wanaDMV na kutaja $1,048 zilizopatikana kutokana namichango ya wanaDMV kwa harambee iliyofanyika kanisani hapo.

Wakati wa sadaka
Kutakiana amani
Wakati wa kupokea.
Picha juu na chini ni kwaya ya Jumuiya ya Katoliki misa ya Kiswahili ikitumbuiza kwenye misa ya kumwombea marehemu Joseph Ndyamukama

Kiboksi kilichobeba majivu ya mpendwa wetu.
Juu na chini ni Padri Honest Munishi akiongoza zoezi la harambe ya kuwezesha kuatikana kwa fadhaza kusaidia familia na kupatikana kwa tiketi ya msindikizaji.
Padri Honest Munishi akiongoza ibada ya marehemu Joseph Ndyamukama na baadae wanaDMV kupata ruksa ya kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.
Padri Honest Munishi akiongoza kutoa pole kwa wafiwa
Picha juu na chini ni wakati wa chakula cha pamoja na wafiwa mara tu baadaya misa kumalizika.
 

No comments: