"IMARISHI VIUNGO TOA MAUMIVU
KWA MAZOEZI LAINI"
Imeandaliwa na Sensei Rumadha Fundi mwalimu wa Karate na Yoga wa kimataifa
Mwili hautofautiani na chombo au mashine, na huitaji sana kuangaliwa na kutunzwa vizuri kana kwamba jinsi mashine inavyofanyiwa matunzo ya kila siku kuwa inafanya kazi imara ipasavyo.
Sawa na ujana wa mwili na nguvu, zinakuwa madhubuti ,lakini, jinsi umri unavyo kuwa, viungo kama magoti, mgongo na miguu navyo huanza kupungua nguvu na kusababisha maumivu ya mwili nzima au baadhi ya viungo.
Hapo basi, mazoezi mepesi ya aina hii, ndio ufumbuzi katika kusaidia kuuweka mwili na viungo vyake katika hali ya afya njema.
Kutokana na ushauri wa wakufunzi wa mazoezi mepesi kama haya, angalau dakika ishirini tu kabla ya kufungua kinywa asubuhi kila siku, inatofautisha sana kulinganisha na mtu anaye fanya mazoezi mazito tu kama kubeba vitu vizito pekee au kutofanya mazoezi kabisa.
Faida kubwa ya haya mazoezi ni ikiwemo utulivu wa mawazo, kumbukumbu za fikra na kimawazo, kuwa na subira na kupunguza hasira za haraka.
Vigezo vikuu vya mazoezi haya mepesi ni kuwa na moyo wa kujitolea katika jitihada za kila siku. Kufanya mazoezi katika mazingira ya usafi, kama vile kuepuka sehemu ya mazoezi yenye vumbi, moshi, kwakuwa mazoezi haya hufanywa katika sakafu kavu na kutandika blanketi.
Mazoezi haya yanaimarisha viungo vya ndani ya mwili " Internal organs " kama vile, figo, mapafu, bandama na moyo. Nidhamu ya mazoezi ni moja ya vitu pekee vinavyo muwezesha mtu kuyafikia haya mafanikio halisi na kupata afya njema.
Mwisho, vyakula vyenye lishe ni muhimu sana, ikiwemo kunywa maji mengi na kupunguza au kuepuka ulaji wa mafuta mengi katika vyakula.
**Sensei Rumadha Fundi **
No comments:
Post a Comment