Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kusikiliza kero za wananchi hao, Juzi 11 Machi 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Wakazi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakimsikiliza Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) wakati wa mkutano wa hadhara, Juzi 11 Machi 2018.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe Ahmed Salum akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo kabla ya kumaribisha Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) kusikiliza kero za wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Juzi 11 Machi 2018.
Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) akiwatuliza wananchi wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ili kusikiliza mgogoro baina ya wananchi hao na kampuni ya Henan Afro-Asia Geo Engineering co ltd kutoka nchini China, Juzi 11 Machi 2018
Naibu waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) (Kushoto) akisikiliza malalamiko kwa baadhi ya Wakazi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kabla ya mkutano wa hadhara uliofanyika Juzi 11 Machi 2018.
Na Mathias Canal, Shinyanga
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto katika ulipaji wa fidia kwa wananchi waliofanyiwa uthamini katika maeneo yao ili kupisha mradi wa uchimbaji wa madini ya dhahabu kupitia kampuni ya Henan Afro-Asia Geo Engineering co ltd kutoka nchini China.
Akizungumza Juzi 11 Machi 2018 na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika Kitongoji cha Mahiga, Kijiji na Kata ya Mwakitoliyo, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) amekiri kuwa zipo changamoto katika jambo hilo hivyo serikali itapitia upya tathimini sambamba na ulipaji wa fidia ili kuhuisha sintofahamu hiyo iliyopelekea wananchi hao kupaza sauti zao za malalamiko.
Mhe Biteko alisema kuwa katika sekta ya madini mnufaika wa kwanza lazima awe mtanzania kwani sheria ya madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaelekeza kuwa na uchumi fungamanishi kwa wananchi ili kuinua pato la wananchi sambamba na mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa.
Aidha, Mhe Biteko aliwasihi wananchi hao kuwa watulivu katika kipindi kifupi ambacho serikali inapitia upya tathmini hiyo huku akiwasihi kuacha uvamizi katika eneo hilo kwani kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.
“Ndugu zangu wananchi Sio kweli kwamba wawekezaji ni wabaya lakini wanapaswa kutambua tu wakija kuwekeza nchini wanapaswa kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ikiwa ni pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na wananchi wanaoishi karibu na mradi huo” Alikaririwa Biteko (Mb)
Machi 10, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wananchi katika eneo la Nyasubi katika Halmashauri ya mji wa Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati wa dhifa ya uzinduzi wa barabara ya Isaka-Ushirombo yenye urefu wa Kilomita 132, alimuagiza Naibu Waziri wa wizara ya madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb) kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe Ahmed Salum kufanya ziara na kuwasikiliza wananchi kuhusu malalamiko hayo ili serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka.
Wananchi hao wanalalamikia kufanyiwa tathmini tofauti na matakwa ya sheria huku wakipatiwa malipo kiduchu pasina kufanyika mkutano wa hadhara wa maridhiano baina ya wananchi na muwekezaji huhu wakiomba kufanyika upya tathmini ya maeneo yao.
No comments:
Post a Comment