ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 10, 2018

HAKUNA CHA AJABU KUFUNGIA NYIMBO ZA WASANII ZILIZOKIUKA MAADILI: DKT. MWAKYEMBE

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe akijibu swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa kumi na moja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Aprili 10, 2018 mjini Dodoma. Dkt. Mwakyembe amesisitiza hakuna ajabu kwa Tanzania kufungia nyimbo za wasanii zilizokiuka maadili kwani hata nchi nyingine kama Nigeria na DR-Congo wamewahi kufanya hivyo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akijibu swali wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa kumi na moja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angela Kairuki (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa kumi na moja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akibalishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Ahmed Juma Ngwali, wakati wa kipindi cha maswali na majibu katika mkutano wa kumi na moja wa bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania, leo mjini Dodoma.

No comments: