Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye mkutano wa Jukwaa la Wanawake ikiwa Sehemu ya mkutano wa Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini London, Uingereza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia na Waziri Mkuu wa Malta Mhe. Dkt. Joseph Muscat mara baada ya mkutano wa Jukwaa la Wanawake kumalizika jijini London, Uingereza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan, jana jioni alikuwa ni miongoni mwa Jopo lililojadili kuhusu sera za kumwinua mwanamke kiuchumi wakati wa mkutano wa Jukwaa la Wanawake linalofanyika kama sehemu ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea hapa London.
Kwenye jopo hilo Mheshimiwa Makamu wa Rais aliungana na Mhe. Dkt. Joseph Muscat, Waziri Mkuu wa Malta na wadau wengine wa masuala ya maendeleo ya wanawake.
Makamu wa Rais aliweza kuelezea hatua mbalimbali ambazo serikali kali imechukua ili kumwinua mwanamke kiuchumi ikiwa pamoja na kuwapatia haki ya kumiliki ardhi, kuboresha elimu kwa mtoto wa kike, kuwapa nafasi za uongozi na pia Serikali ipo kwenye hatua za kuhakikisha mikopo yenye riba nafuu kwa Wanawake.
Makamu wa Rais yupo jijini London kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola.
No comments:
Post a Comment