JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
9 Barabra ya Ohio
S. L. P.
5821,
DAR ES
SALAAM.
|
|
Simu Nambari: +255-22-2113537
Nukushi: + 255-22-2184569
Barua Pepe: fire.rescue@frf.go.tz
TAARIFA
KWA UMMA
Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji linapenda kutoa taarifa kwa umma kufuatia tukio la moto kwenye ukumbi wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililotokea mnamo tarehe 09 Aprili,
2018 majira ya saa 1:28 usiku mkoani Dodoma.
Uchunguzi wa awali
unaonyesha kuwa moto huo ulisababishwa na shoti iliyotokana na Power bank iliyokuwa inatumiwa kuchaji
simu. Shoti hiyo ilisababisha kuungua kwa simu, Power bank, sehemu ya meza na kapeti kitendo kilicholeta moshi
mkubwa na taharuki miongoni mwa Wabunge. Ukiachilia mbali taharuki kwa
Waheshimiwa Wabunge hakuna madhara kwa binadamu yaliyotokana na moto huo.
Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa rai kwa Watanzania wote kuchukua tahadhari
kubwa hasa wanapokua wanatumia vifaa vya kieletroniki ambavyo kwa sasa vipo
katika matumizi hadi katika ngazi ya familia. Moto huzuka tu endapo
kitapatikana chakula cha moto, joto la kutosha na hewa ya oksijeni (fuel, heat and oxygen).
Sambamba na hayo
Kamishna Jenerali anahimiza uzingatiaji wa kinga na tahadhari ya moto katika
maeneo yote. Wamiliki wa maeneo ya umma, binafsi na biashara wanapaswa kufunga
vizimia moto kwa kuzingatia ushauri unaotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji lipo imara na litaendelea kuwaelimisha Watanzania kuzingatia kinga na
tahadhari ya moto ili kuhakikisha maisha na mali vinakuwa salama.
Imetolewa na;
CGF.
Thobias Andengenye
Kamishna Jenerali
Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji
10 Aprili, 2018
No comments:
Post a Comment