Na
Mwandishi Wetu
Mkurugenzi
na Mmilikiwa kampuni ya PAP/IPTL ,Harbinder Sing Sethi Amekanusha taarifa
zinazosambzwa mitandao kuwa amefutwa kuwa Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa
kampuni hiyo.
Hayo
yameelezwa leo na Mwanasheria wa mmiliki wa Kampuni ya PAP/IPTL, Harbinder
Sing Sethi, Hajra Mungula, mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mteja wake na
kusema Sethi bado Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.
Wakili
Mungula amesema kuwa watanzania kupuuza kwa taarifa zilizotolewa
awali na watu wanaojiita kuwa Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
hiyo.
Katika
taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Wakili Hajra Mungula imesema kuwa yeye kama mwanasheria wa Sethi, amewasiliana
na mteja wake, ambaye yuko rumande na kushangazwa na taarifa hizo.
Ilisema
hivi karibuni kumeripotiwa taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba kampuni
inayomilikiwa na Harbinder Sing Sethi imebadilisha uongozi katika ngazi za
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Mkurugenzi mtendaji wake.
"Taarifa
iliyosambazwa na anayejiita mwenyekiti wa bodi mpya, Ambroce Brixio imemtaja
yeye kuwa na cheo hicho na Joseph Makandege kuwa Mkurugenzi wake ambaye kwa
miezi kadhaa sasa hajawahi kuonana nae ikiwemo hata kutofika mahakamani siku ambazo
kesi imekuwa ikitajwa" imesema sehemeu ya taarifa hiyo.
Wakili
Hajra, aliandika katika taarifa hiyo kuwa taarifa hizo zimemfikia kwa
masikitiko makubwa Mwenyekiti halali na mmiliki wa kampuni hii ya kuzalisha
umeme ya IPTL ambayo kimsingi inamilikiwa na kampuni anayoimiliki ya Pan Africa
Power Solutions(PAP).
Kwa
mujibu wa taarifa ya mwanasheria huyo, pamoja na kuagiza wanasheria wake
kuchukua hatua za haraka za kisheria mwenyekiti Sethi pia hana taarifa zozote
juu ya mabadiliko hayo.
"Mwenyekiti
Seth anapenda kuutaarifu umma kupitia sisi kwamba wazipuuze taarifa hizo kwa
kuwa hazitokani na mamlaka halali za kisheria za kampuni hiyo," ilisema
mwanasheria huyo.
Ilisema
pamoja na kwamba Mwenyekiti Sethi bado yuko mahabusu akituhumiwa mashtaka
kadhaa ya jinai, hiyo haiondoi ukweli kuwa IPTL ni kampuni binafsi yenye
wamiliki halali wenye hisa halali na wala sio NGO ambayo mtu yeyote anaweza
kutangaza mapinduzi ya kiuongozi wakati wowote.
"Mwenyekiti
anapenda kuwahakikishia watanzania wote kuwa licha ya uwepo wa mashtaka
yanayomkabili bado kampuni hiyo ipo chini ya usimamizi salama wa PAP na kwamba
madeni yote, madai, mali na stahiki zote zizohusiana na kampuni hiyo zipo
katika mikono salama mpaka sasa" ilisema sehemu ya taarifa
Aidha,
ilisema taarifa hiyo, Mwenyekiti anawahakikishia watanzania kuwa ataendelea
kutoa ushirikiano mahsusi kuhakikisha nchi inajiepusha na hasara zinazotokana
na matendo ya aina ya kina Makandege na wenzake ya kukurupuka bila kufuata
sheria na taratibu
No comments:
Post a Comment