Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta binafsi na Umma, kutoka Wizara
ya Fedha na Mipango Dkt. John Mboya, akizungumzia faida za miradi ya
ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi wakati wa semina kwa wajumbe wa
Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji
Mitaji ya umma, iliyofanyika Jijini Dodoma.
Wataalamu washauri wa masuala ya Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya
Umma (PPP) Bw. Abhijit Bhaumik (kushoto), Bw. Philip Kelly (katikati)
na Bw. Craig Sugden, wakijadiliana jambo wakati wa semina ya Kamati tatu
za Bunge za Bajeti, Miundombinu na Uwekezaji Mitaji ya Umma,
iliyofanyika Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu,
akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za
Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji Mitaji ya Umma, ilifanyika
Jijini Dodoma kuhusu hatua zilizochukuliwa na taasisi hiyo za kupanga
kujenga viwanda vitatu vya dawa na vifaa tiba kwa kuishirikisha Sekta
Binafsi (PPP).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC)
Mhandisi Kapuulya Musomba, akiwasilisha mada kwa wajumbe wa Kamati za
Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji Mitaji ya
Umma, Jijini Dodoma, kuhusu hatua zilizochukuliwa na Shirika hilo
kutaka kuishirikisha Sekta Binafsi kutekeleza mradi mkubwa wa
kuunganisha gesi majumbani katika katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi
na Mtwara kupitia ubia kati na sekta binafsi na Umma (PPP) utakaogharimu
zaidi ya shilingi bilioni 300.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na
ile ya Mitaji ya Umma wakifuatilia semina kuhusu dhana ya utekelezaji
wa miradi ya maendeleo kwa njia ya ubia kati ya sekta binafsi na umma
(PPP), Jijini Dodoma
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba
Ndaki (Mb), akizungumzia matarajio ya wabunge katika utekelezaji wa
miradi ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi katika kuchochea
maendeleo, wakati wa semina kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za
Miundombinu, Bajeti na kamati ya Uwekezaji Mitaji ya Umma, iliyofanyika
Jijini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti
na Uwekezaji na Mitaji ya Umma wakifuatilia semina kuhusu dhana ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa njia ya ubia kati ya sekta
binafsi na umma (PPP), Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Bariadi Mhe. Andrew Chenge (kulia) na
Mbunge wa Ileje Mhe. Dkt. Janeth Mbene, wakifuatilia kwa makini mada
mbalimbali zilizotolewa na wataalam kutoka Benki ya Dunia kuhusu masuala
ya utekelezaji wa Miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta
Binafsi, Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFP)
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
WAJUMBE wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji na Mitaji, wameishauri Serikali kutekeleza kwa vitendo miradi mikubwa na yenye tija kwa Umma kwa kutumia njia ya Ubia kati ya Umma na Sekta binafsi ili kuchochea haraka maendeleo ya nchi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki amesema kuwa wabunge wameridhishwa na na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa mpango wa ubia kati ya Serikali na sekta binafsi unafanikiwa na unachochea maendeleo ya wananchi.
“Kama wabunge tungependa kuona mpango unaingizwa katika mipango ya Serikali ili kuharakisha miradi ya maendeleo na pia tunapongeza hatua zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo kumteua Kamishna anayeshughulikia miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ile ya umma, “ Alisisitiza Mboya
Alibainisha kuwa jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wote watakaojitokeza kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo hapa nchini.
Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mhe. Endrew Chenge amesema kuwa nchi nyingi Duniani zimefanikiwa kuwaletea wananchi wake maendeleo kupitia utaratibu huo ambapo jambo la muhimu ni kufanywa kwa maandalizi ya kina na kuwepo kwa utashi kutasaidia kufanikiwa kwa miradi husika .
Aliongeza kuwa mwaka huu Serikali imeleta Bungeni Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya PPP utakaojadiliwa na wabunge katika Bunge linaloanza Septemba 4 mwaka huu, pamoja na mambno mengine Muswada huo unapendekeza kuanzishwa kwa Kituo cha PPP chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, ambacho kitakuwa na jukumu la kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayo husu miradi mbalimbali itakayowasilishwa kwa mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
Akizungumza katika Semina hiyo, Kamishna wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. John Mboya amesema kuwa Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi katika kutekeleza miradi ya ubia na Sekta binafsi ili kuleta mageuzi katika maisha ya wananchi.
“Lengo la kuwa na miradi ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi ni kutekelezaIilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza mpango wa maendeleo na hatimaye kutoa huduma bora kwa wananchi,” Alisisitiza Mboya
Akifafanua Mboya amesema kuwa moja ya hatua za maboresho zilizochukuliwa na Serikali ni kuhamisha Kituo cha kusimamia miradi ya ubia katika ya Umma na Sekta binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuja Wizara ya Fedha.
Akizungumzia majukumu ya chombo cha kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo Dkt. Mboya amesema kuwa chombo hicho kimepewa jukumu la kufanya uchambuzi wa kina kuhusu miradi yenye sifa na kusimamia mchakato wa uteklezaji wa mpango huo kwa kufuata ngazi zote zilizopo hadi utekelezaji wa mradi husika.
Aliongeza kuwa ili kufanikisha mpango huo Serikali inasisistiza uwazi, uwajibikaji na utayari hali itakayo sababisha kufikiwa kwa malengo ya miradi ya ubia kati ya sekta hizo mbili ambapo alitaja baadhi ya miradi itakayotekelezwa ambayo upembuzi yakinifu umekamilika kuwa ni ile ya ujenzi wa Viwanda vya dawa, usambazaji wa gesi majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara , Lindi na ule wa uendeshaji wa mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar es Salaam ambao umeanza na uko katika hatua mbalimbali za uendelezwaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu amesema kuwa tayari Bohari hiyo imekamilisha upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba vinavyotokana na malighafi zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo pamba na kufikia machi mwakani zabuni ya mradi huo itatangazwa ili kuwapata wabia.
Katika kutekeleza mradi huo kiwanda cha kuzalisha maji ya dripu yanayotumika kwa wagonjwa mahosipitalini pia kitajengwa ambapo kwa sasa maji hayo yanaagizwa kutoka nchini Uganda na kwamba hatua hiyo itapunguza gharama za Serikali za kuagiza dawa na vifaa hivyo kutoka nje ya nchi ambapo zaidi ya shilingi trilioni 1.8 hutumika kuagiza bidhaa hizo kila mwaka.
Kwa upande wake. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba amesema kuwa mradi wa kusambaza gesi majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara na Lindi unaotarajiwa kuhgaribu zaidi ya shilingi bilioni 300, utaleta mageuzi kwa wananchi wa mikoa hiyo ambapo wananchi zaidi ya 120,000 katika Jiji la Dar es Salaam watafikiwa.
Aliongeza kuwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara wananchi zaidi ya 5,000 wataunganishiwa gesi majumbani mwao huku viwanda zaidi 30 katika maeneo ya mradi vitaunganishiwa huduma hiyo pamoja na vituo vya kujaza gesi kwenye magari yanayotumia nishati hiyo.
Semina kwa wabunge wa Kamati za Bajeti, Miundombinu na ile ya Uwekezaji Mitaji imefanyika Jijini Dodoma ikiwashirikisha wajumbe wa Kamati hizo ili kuwajengea uwezo wa namna dhana hiyo inavyoweza kuleta maendeleo hapa nchini.

No comments:
Post a Comment