Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela
(wakwanza kulia) akiwaongoza wafanyakazi wa Mamlaka hiyo, Mkurugenzi wa Kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa chas Julius Nyerere (JNIA) Bw. Paul Rwegasha (watatu
kulia) na Afisa Uhusiano Bi. Bahati Mollel (wapili kulia) kukabidhi mfano
wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 5 (5,000,000/=) kwa mgeni rasmi
kwenye hafla ya bunge kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule nchi
nzima, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne
Makinda (wapili kushoto) na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo,
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka. Hafla hiyo ilifanyika usiku wa
kuamkia leo Septemba 1, 2018 jijini Dar es Salaam.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMLAKA
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeunga mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, kupitia Umoja wa Wabunge Wanawake wa Bunge hilo, (TWPG)
kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga vyoo salama vya shule nchi nzima kwa mtoto
wa Kike kwa kutoa mchango wa kiasi cha Shilingi Milioni Tano (5,000,000).
Katika
hafla ya kuchangisha fedha kwa dhumuni hilo, iliyofanyika katika ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela, alikabidhi msaada huo wa fedha kwa mgeni
rasmi, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne
Makinda.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa (TWPG), ambaye pia ni Mbunge wa Urambo, Mhe.Margareth
S. Sitta, wazo la kutafuta fedha za ujenzi wa vyoo hivyo ni katika jitihada za
kuhakikisha wanafunzi wote hususan wa kike, wanafurahia haki yao ya msingi ya
kupata elimu katika mazingira rafiki na masafi bila kujali changamoto
zinazosababishwa na tofauti zao za kimaumbile.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Wabunge, Wakuu
wa Taasisi za Umma na Binafsi, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, aliwapongeza
Wabunge hao kwa hatua hiyo ya kuhakikisha kunakuwepo kwa mazingira bora shuleni ili kutoa haki sawa ya
kupata elimu kwa wanafunzi wote.
“Wazo
hili litasaidia sana serikali katika kuhakikisha mazingira ya shule
yanaboreshwa ili kutoa nafasi sawa kwa wanafunzi wote wa kike na kiume”
alibainisha Spika Ndugai.
Alisema
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,
amefurahishwa sana na kitendo hicho na kwamba ameshindwa kuhudhuria hafla hiyo
kwa vile bado yuko kwenye msiba wa dada yake huko Chato Mkoani Geita.
Kwa
upande wake, mgeni rasmi Mhe. Anne Makinda aliwapongeza wabunge hao wanawake
kwa hatua hiyo ya kuunga mkono juhudi za serikali na kuwataka Wabunge wanaume
kuwaunga mkono wenzao katika kufanikisha kampeni hiyo inayolenga kukusanya
kiasi cha shilingi bilioni 3.5 zitakazowezesha kujenga vyoo vya shule kwenye
majimbo yote 264 nchi nzima.
Taasisi
mbalimbali zilichangia kwenye harambee hiyo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, akizunhgumza.
Mwenyekiti wa Kundi la Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Urambo, Mhe. Margareth S. Sitta, akitoa hotuba yake.
Mgeni rasmi kwenye hafla ya bunge kuchangisha
fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule nchi nzima, Spika mstaafu wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda, akitoa nasaha zake.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo,
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, akitoa nasaha zake.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela, akifuatilia kilichokuwa kikizungumzwa na viongozi.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha akifurahia jambo.
Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wakifuatilia hafla hiyo.
Meza ya wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji nchini.
Spika Ndugai akiongoza wabunge wengine kusakata rhumba
Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni msanii wa muziki, Mhe. Martha Mlata akiimba kwenye hafla hiyo.
Wabunge wa Viti Maalum wakisakata rhumba.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, akiongozana na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson wakati wakiingia ukumbini. |
Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kiwkete akiwa na Mbunge wa jimbo la Segerea, Mhe. Bonner Kalua
No comments:
Post a Comment