Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo akiwasili kwenye ukumbi wa American Corner akiwa ameambatana Mwanzilishi mwenza wa Apps & Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Lyra in Africa, Bi. Roselyne Mariki (katikati) wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa Shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika jana katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo akizungumza kutia hamasa wasichana wa shule mbalimbali za sekondari nchini wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa Shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika jana katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Mtaalamu wa Mawasiliano katika Sekta ya Nishati kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanazania, Johary Kachwamba akiwasilisha fursa za ubunifu katika sekta ya nishati wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika jana katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Afisa Mipango wa Reach for Change Foundation, Bi. Jesca Mmari akizungumza na wanafunzi akiwataka kuwa na hamu na kujiamini katika kila kitu wanachotaka kukipata wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika jana katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Mtalaamu wa Jinsia na Vijana kutoka Shirika la Misaada la Marekani nchini (USAID), Bi. Shamsa Suleiman akizungumzia kazi mbalimbali zinazofanywa na shirika lake wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Afisa Rasilimali watu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. John Mtega (kushoto) akizungumzia usawa wa kijinsia katika ajira na kuhamasisha wanawake kuomba nafasi za utumishi wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mhandisi wa Umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bi. Mkufu Shabaan (wa pili kushoto), Mtalaamu wa Jinsia na Vijana kutoka Shirika la Misaada la Marekani nchini (USAID), Bi. Shamsa Suleiman (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mipango wa Reach for Change Foundation, Bi. Jesca Mmari (kulia).
Wakili kutoka TLS Dar es Salaam Chapter, Angelista Nashon akizungumzia haki za mabinti katika jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali 2018 (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo (kulia) akisalimiana na Mtalaamu wa Jinsia na Vijana kutoka Shirika la Misaada la Marekani nchini (USAID), Bi. Shamsa Suleiman wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Lyra in Africa, Bi. Roselyne Mariki.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo (wa pili kulia) akifurahi jambo na Mtalaamu wa Jinsia na Vijana kutoka Shirika la Misaada la Marekani nchini (USAID), Bi. Shamsa Suleiman (kushoto) wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Lyra in Africa, Bi. Roselyne Mariki (wa pili kushoto) pamoja na Mwanzilishi mwenza wa Apps & Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima (kulia).
Mkurugenzi wa Lyra in Africa, Bi. Roselyne Mariki akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Lyra in Africa, Bi. Roselyne Mariki.
Afisa anayeshughulikia Utamaduni kutoka Ubalozi wa Marekani, Bw. Jeffrey Ladenson (kushoto) akiteta jambo na Wakili kutoka TLS Dar es Salaam Chapter, Angelista Nashon (kulia) wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mhandisi wa Umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bi. Mkufu Shabaan
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa elimu na baadhi ya wanafunzi walioshiriki jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani lililomalizika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Washindi wa kwanza wa shindano la ubunifu wa programu za kompyuta, ambao waliwasilisha wazo la changamoto za ukosefu wa taulo za watoto kike mashuleni wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa anayeshughulikia Utamaduni kutoka Ubalozi wa Marekani, Bw. Jeffrey Ladenson (wa tatu kushoto), Mwanzilishi mwenza wa Apps & Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima (kushoto) na majaji wa shindano hilo wakiongozwa na Jaji Kiongozi wa shindano hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Lyra in Africa, Bi. Roselyne Mariki (wa tatu kulia) wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Washindi hao ni Eshe Mohamed (wa pili kushoto), Oliver Godliving (wa nne kushoto), Maleo Stanley (wa tano kulia) pamoja na Mwalimu Msimazi, Celestina Richard (wa nne kulia) kutoka shule ya Sekondari Kondo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Washindi wa pili wa shindano la ubunifu wa programu za kompyuta, ambao waliwasilisha wazo la kutengeneza programu itakayowarahisishia wanafunzi wapya kutambua maeneo ya makazi ya kupangisha yaliyokaribu na vyuo wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa anayeshughulikia Utamaduni kutoka Ubalozi wa Marekani, Bw. Jeffrey Ladenson (wa pili kushoto), Mwanzilishi mwenza wa Apps & Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima (kushoto) pamoja na majaji wa shindano hilo wakiongozwa na Jaji Kiongozi wa shindano hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Lyra in Africa, Bi. Roselyne Mariki (wa tatu kulia) wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Washindi hao ni Sia Nicholaus (wa nne kushoto), Rahma Habibu (wa tatu kushoto), Raphia Mohamed (wa nne kulia) pamoja na Mwalimu msimamizi, Nsia Shoo (katikati) kutoka shule ya Sekondari ya Jamhuri jijini Dar es Salaam.
Washindi wa tatu wa shindano la ubunifu wa programu za kompyuta, ambao waliwasilisha wazo la kupunguza ajali za barabarani wakiwa katika picha ya pamoja na Afisa anayeshughulikia Utamaduni kutoka Ubalozi wa Marekani, Bw. Jeffrey Ladenson (wa pili kushoto), Mwanzilishi mwenza wa Apps & Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima (kushoto) pamoja na majaji wa shindano hilo wakiongozwa na Jaji Kiongozi wa shindano hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Lyra in Africa, Bi. Roselyne Mariki (wa tatu kulia) wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali la ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam. Washindi hao ni Nelusigwe Komba (wa nne kushoto), Fatuma Magogo (wa tatu kushoto), Rannifelucy Rodgers (wa nne kulia) pamoja na Mwalimu Msimamizi, Musa Roche (katikati) wakiwa na zawadi zao za simu janja ‘Smart Phones’ kila mmoja wakitokea Shule ya Sekondari Gerezani ya jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi wetu
MKUU wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wasichana kutumia fursa za uwapo wa Tehama kutimiza ndoto zao.
Ushauri huo aliutoa mwishoni mwa wiki wakati alipozungumza na wasichana wa sekondari waliokuwa katika jukwaa la ujasiriamali kwa wasichana.
Jumla ya wasichana 156 kutoka shule 25 za Dar es salaam walijumuika kwa siku mbili katika jukwaa ambapo miradi yao iliyobuniwa kwa kutumia teknolojia ilifanyiwa uhakiki na mshindi kupewa tuzo.
Katika jukwaa hilo lililoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Apps and Girls likishirikiana na Ubalozi wa Marekani hapa nchini, Jokate Mwegelo alisema wasichana wa nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko katika maisha yao na jamii zao wanachotakiwa ni kutumia fursa zilizopo vizuri.
Alisema mafunzo ambayo wasichana hao wameyachukua ni fursa nzuri ya kujibadilisha na kusema hawana sababu ya kuwa waoga katika hilo bali wajitume inavyostahili.
Alisema katika utekelezaji wa ndoto zao kunakuwa na vikwazo vingi lakini ni wajibu wao kuvishinda na kusonga mbele.
Alitolea mfano yeye ambapo baada ya kusoma alisimama kidogo na kuwaambia wazazi wake kwamba anasimama kidogo ili atengeneze bidhaa ambazo zingeweza kumfanya kutimiza ndoto yake.
Alisema japokuwa wazazi wake hawakumwelewa alikazania alichofikiri na ndio chanzo cha kidoti, alama inayotambuliwa na watu wengi.
Alisema baada ya mafunzo yao ni vyema wakatambua na kujitambua wao wanaweza nini ili waweze kuwa juu.
“Haiwezi kuwa rahisi hata Yesu alibeba msalaba wake kukomboa watu wake” alisema akimaananisha kwamba ni vyema kuwa na maono ya unachotaka kama unataka kushiriki vyema.
Alisema kwamba wamejifunza elimu ya dijiti kama vile programu za Kompyuta (coding) na ujasiriamali wanachotakiwa kukifanya ni kufanya ubunifu wa miradi inayohusisha teknolojia na kuitumia mitandao ya kijamii kwa manufaa yao kwa kuwa mitandao inaunganisha dunia.
Alisema kwamba kama mtoto wa kike akijielewa atatumia vyema fursa za uwekezaji zilizopo kwa kutumia vyema elimu anayoipta na kujiingiza katika ujasiriamali.
“Mafunzo yawabadili, yawafanye muwe na msimamo” alisema Jokate ambaye pia aliwashukuru watu wa ubalozi wa Marekani kwa kumona fursa ya kuzungumza kuwatia hamasa mabinti hao kwamba inawezekana.
Alisema wakati umefika kwa wasichana hao kutumia Tehama kujiunga na dunia na kufanya yale ambayo wameyapanga katika maisha yao na kufanikiwa.
Sambamba na hutuba hiyo ya hamasa kulikuwa na siku mbili, za jukwaa katika ukumbi wa American Corner katika Maktaba Kuu ya Taifa.
Washindi wa ujasiriamali walipewa zawadi zao baada ya kumaliza mafunzo na mchujo kufanyika.
Katika kufanikisha mafunzo haya, shirika la Apps and Girls liliweka ushirikiano wa karibu na waalimu wa shule husika ikiwa ni pamoja na kuendesha semina kwa waalimu kuhusu umuhimu wa tehama kwa wanafunzi.
Pia walimu waliweza kuanzisha vilabu vya kompyuta (coding clubs) ambapo wanafunzi walipata kutembelewa na wakufunzi kutoka Apps and Girls kwa siku maalumu za vilabu mashuleni.
Moja kati ya mafunzo wanayoyapata wasichana kutoka Apps and Girls ni pamoja na program za kompyuta kama vile MTHL, Java, Scratch na Arduino. Hizi ni programu adhimu za kompyuta zinazomuwezesha mwanafunzi kutengeneza tovuti, application za simu pamoja na kutengeneza roboti.
Shirika la Apps and Girls linalenga kuziba pengo lililopo ambapo wasichana na wanawake kwa ujumla wako nyuma katika elimu ya dijiti na sayansi kwa ujumla. Hivyo shirika hilo linatoa elimu ya programu za kompyuta bure kwa watoto wa kike ili kuwawezesha kupata maarifa ya kidijitali na kuondoa pengo lilopo kwa sasa.

No comments:
Post a Comment