ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 28, 2018

OFISI YA WAZIRI MKUU WASAINI MIKATABA NA MAKAPUNI YA VIJANA YATAKAYOTOA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Peter Kalonga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba na makampuni ya vijana yatakayoanza kujenga na kutoa mafunzo ya kilimo kupitia kitalu nyumba Novemba 27, 2018 Jijini Dodoma. 
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Peter Kalonga akisaini Mikataba ya Ujenzi na utoaji mafunzo ya Kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House) kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, (pembeni yake) ni Meneja Mwendeshaji wa SUGECO naye akisaini mikataba hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Peter Kalonga wakibadilishana mikataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Royal Agri Company Ltd Bw. Jonathan Sangau mara baada ya Kusaini hii leo Novemba 27, 2018 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Ajira Bw. Ally Msaki akielezea jambo wakati wa hafla hiyo ya utiaji saini wa mikataba na makampuni ya vijana yatakayoanza kutoa mafunzo ya kilimo kupitia kitalu nyumba iliyofanyika Jijini Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Holly Green Agric Ltd, Eng. Octavian Lasway akizungumza jambo na washiriki wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akifafanua jambo kuhusu vijana wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. (Kushoto) ni Mkurugenzi wa Idara ya Ajira Bw. Ally Msaki.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa ofisi hiyo na wawakilishi wa makampuni hayo wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Peter Kalonga.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa ofisi hiyo na wawakilishi wa makampuni hayo wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Peter Kalonga.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Peter Kalonga akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa ofisi hiyo na wawakilishi wa makampuni yatakayoanza ujenzi na kutoa mafunzo ya kilimo kupitia kitalu nyumba mara baada ya hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma.

No comments: