Mrembo Vanessa Ponce de Leon kutoka nchini Mexico ameibuka mshindi wa taji la mrembo wa dunia 2018 kwenye shindano lililomalizika jioni hii huko nchini China. Ponce mwenye umri wa miaka 26, amekuwa Miss World wa 68 tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Washiriki 118 wa taji la Miss World 2018 akiwemo Mtanzania, Elizabeth Makune ‘Queen Elizabeth’walikuwa wakichuana kuwania taji hilo ambapo wamepita katika michujo mbalimbali wakati wa hafla za kumsaka mshindi hii leo lakini Vanessa amewaburuza wote na kuibuka mshindi.
Katika tukio hilo lililofanyika Sanya City Arena, mshindi wa Miss World 2017, Manushi Chhillar kwa furaha ndiye alimvalisha taji Vanessa kama ishara ya kumkabishi kijiti cha umalkkia wa urembo wa dunia kwa mwaka 2018. GPL
No comments:
Post a Comment