Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Meneja wa Mpango wa
Taifa Chanjo, Dk. Dafrossa Lyimo akizungumza kwenye hitimisho la semina maalum kwa waandishi wa habari mbalimbali,juu ya uelewa wa Chanjo hapa nchini. Tukio lililofanyika mapema leo Jijini Dar es Salaam.
NA Andrew Chale.
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na
Watoto kwa kushirikiana na Wadau wengine wakiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO)
mapema leo wameendesha semina maalum kwa Waandishi wa Habari juu ya uelewa wa
Chanjo zinazotolewa hapa nchini, tokea kuanzishwa kwake mwaka 1975.
Tanzania walianza kutoa Chanjo aina tano (5) pekee, lakini mpaka kufikia sasa imevuka hatua
na kufikia kutoka aina 15 za Chanjo. Wizara ya Afya katika mpango wake
, inasisitiza wazazi kuhakikisha watoto
wao wanapata chanjo zote zinazotakiwa kwa wakati ili waweze kuepukana na magonjwa mbalimbali.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Meneja wa Mpango wa
Taifa Chanjo, Dk. Dafrossa Lyimo amesema
kuwa chanjo ni bure na inapatikana kila
Zahanati, vituo vya afya na maeno husika hivyo wahitajika wa Chanjo wanatakiwa
kupelekwa nakupatiwa wakiwemo watoto ambao ndio wenye uhitaji mkubwa .
“Chanjo ni bure. Lakini kuna watu wamekimbia chanjo, ndio
maana tunawaomba wanahabari mtusaidie kutoa elimu ili watu wakapate chanjo. Na tungependa kila baada ya miezi mitatu
tukutane na nyie Wanahabari. Tunawaomba mtufikishie hizi habari kwa Club zenu
za Wanahabari ili taarifa za Chanjo zienee kote” alisema Dk. Dafrossa Lyimo
akisisitiza kwa Wanahabari.
Akielezea ugonjwa wa Surua na Rubella, alifafanua kuwa, ugonjwa huo unafanana
lakini kwa Rubella wamama wanaoshika ujauzito, madhara yake ni kwa mototo
atakayezaliwa kuwa na shida kwenye ini, ana tundu kwenye moyo, figo na maeneo
mengine.
“Surua na Rubella dalili zake zinafanana kwa karibu sana. Unaweza
kuja na dalili za surua, lakini mpaka ufanye vipimo kwa ukaribu sana ndio
unakuta ni Rubella lakini chanjo zake ni moja lakini ni magonjwa mawili tofauti
yaani surua na Rubella.” Alieleza Dk. Dafrossa Lyimo wakati wa kufafanua
ugonjwa wa Surua na Rubella.
Akielezea ugonjwa wa Polio, amebainisha kuwa, kwenye ugonjwa
mmoja anaweza kuambukiza watu zaidi ya 2,00 ndio
maana wanahamasisha watu wapate chanjo
ilikuepuka matitizo kwani tatizo
la ugonjwa huo upotez pia nguvu kazi ya Taifa.
Adiha, Dk.Dafrossa Lyimo amewataka Waandishi wa habari
kuzingatia na kuacha mazoea, Chanjo
haipo kwenye kidonge, bali chanjo ipo kwenye mfumo wa sindano ama tone (maji )
na mfumo huo mpaka sasa haujabadilishwa.
“Mtu akikuletea kidonge akikuambia chanjo hiyo sio chanjo, hiyo ni kinga tiba na unaweza kunywa muda
wowote mfano dawa ya kinga ya minyoo ama mabusha hiyo haina ratiba kila mwaka
unakunywa, ya kwetu Chanjo ina muda maalum.” Alieleza Dk. Dafrossa Lyimo.
Pia amewataka Jamii kuzingatia kumaliza dozi za kinga kwa
wakati hii ni kwa kufuata ratiba watakazowekewa na watalaam.
Dk. Dafrossa Lyimo
amebainisha kuwa, Chanjo ni haki ya kila mototo, hivyo wanatakiwa wapeleke kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
akapate chanjo.
Imeelezwa kuwa, chanjo siyo tu zinaokoa maisha, bali
uboresha maisha pia huku kwa mwaka huu kauli mbiu ikiwa: “Chanjo ni kinga, kwa pamoja tuwakinge” .
Nae Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Mtalaam wa
Chanjo, Dk. William Mwengee amebainisha kuwa, Tanzania imepiga hatua katika
masuala ya chanjo kwa kuweza kuhakikisha chanjo inafika kwa wakati karibu
maeneo yote licha ya changamoto ya usafiri ama wa kifedha inayotokea baadhi ya
maeno ya Nchi kutokana na hali halisi ya wakati huo.
Dk Mwengee ameongeza kuwa, Tanzania ni moja kati ya nchi
ambazo zinachukua hatua ya kuwa na chanjo ili kuhakikisha kuwa maradhi
yanayozuilika hayaendelei kuwa tatizo tena na kuhakikisha kwamba watoto wote
wanaozaliwa hospitalini au nje ya hospitali wanapata huduma zote za chanjo kama
ilivyo pangwa ambapo imeweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.
“Magonjwa yanayodhuilika ya chanjo, yanaua, tena yanaua kwa
kiwango kikubwa sana, hivyo tunao wajibu wa kutumia kalamu zetu kupaza sauti
juu ya watu wakapate chanjo” alieleza Dk. Mwangee.
Kila mwezi wa Nne (Aprili) ni wiki ya Chanjo Barani Afrika,
ambapo jamii imetakiwa kuhakikisha motto
anakamilisha chanjo. Ambapo chanjo hiyo uwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa Polio, Surua, Rubella, Kuhara,
donda koo, Kifaduro, Pepopunda, homa ya ini, kifua kikuu, Homa ya Uti wa
mgongo, Nimonia na mengine mengi.
Watalaam hao wameweka wazi kuwa, Mtoto asiyepata Chanjo, ni
hatari kwa maisha yake na jamii inayomzunguka sababu anaweza kuambukizwa
magonjwa na kuambukiza wengine.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Mtalaam wa Chanjo, Dk. William Mwengee akizungumza katika semina hiyo kwa wanahabari
Mwanahabari James Kandoya wa The Guardian, akiuliza swali kuhusiana na masuala ya Chanjo
Wanahabri wakijadili mada kwenye semina hiyo
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Mtalaam wa Chanjo, Dk. William Mwengee akiteta na mwandishi wa habari wa THE CITIZEN, John NK.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Meneja wa Mpango wa Taifa Chanjo, Dk. Dafrossa Lyimo akizungumza kwenye hitimisho la semina maalum kwa waandishi wa habari mbalimbali,juu ya uelewa wa Chanjo hapa nchini. Tukio lililofanyika mapema leo Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Mtalaam wa Chanjo, Dk. William Mwengee akizungumza katika semina hiyo kwa wanahabari
Mtaalamu wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya, Lotalis Gadau akizungumza katika semina hiyo |
No comments:
Post a Comment