ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 24, 2019

Mshiriki kutoka Mwanza atwaa taji la Miss Tanzania


By Nasra Abdallah, Mwananchi

Dar es Salaam. Hatimaye fainali za Miss Tanzania 2019 zimefikia tamati huku taji la shindano hilo likinyakuliwa na Kanda ya Ziwa.

Shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia leo Jumamosi Agosti 24,2019 lilifanyika katika ukumbi wa Kisena Millennium Tower, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi.

Wengine waliohudhuria ni aliyewahi kuwa waziri wa maliasili na utalii, Lazaro Nyalandy na baadhi ya warembo waliowahi kushiriki shindano hilo miaka ya nyuma akiwemo Miriam Odemba.

Shindano hilo lililoanza saa 4:20 usiku wa jana Ijumaa lilifikia tamati saa saba usiku wa kuamkia leo Jumamosi baada ya Silvia Sebastian kutokea Mkoa wa Mwanza na mwakilishi kutoka Kanda ya Ziwa akiibuka mshindi.

Jina la Silvia lilitangazwa na Jaji Mkuu wa shindano hilo, Shyarose Bhanji, jambo lililoibua shangwe na nderemo kwa ndugu jamaa na marafiki wa mrembo huyo huku mwenyewe akibubujikwa na machozi.

Kutoka na ushindi huo, Silvia ameondoka na kitita cha Sh10 milioni huku mshindi wa pili Grayres Amos akiondoka na sofa yenye thamani ya Sh2 milioni na mshindi wa tatu Qeen Antony akiondoka na Sh1 milioni moja.

No comments: