ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 22, 2019

Mama wa bilionea Msuya akubali kufuta kesi ya kuomba usimamizi wa mirathi

Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Jerry Muro akiwa mbele ya nyumba ya marehemu Bilionea Msuya akiwa amewakutanisha baba wa bilionea MsuyaErisaria Msuya,Mama Ndedhukuro Sikawa na mjukuu wao,Kelvin Msuya ambao kwa muda mrefu walikuwa hawazungumza,baada ya kuagiza warejeshwe watoto katika nyumba ya wazazi wao. Picha Mussa Juma wa ufupi

By Mussa Juma, mwananchi Mjuma@mwananchi.co.tz

Arusha. Hatimaye mama wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Ndeshikurwa Sikawa aliyekuwa amefungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kuomba Miriam Mrita ambaye ni mjane wa bilionea huyo kuondolewa kusimamia mirathi, amekubali kuondoa kesi hiyo ili kusaka maridhiano.

Uamuzi huo, umefikiwa Jumatatu, Octoba 21 2019, katika kikao cha kusaka suluhu katika mgogoro wa kugombea mali za bilionea huyo, baina ya watoto wake na ukoo wa Msuya kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro.

Mama huyo alikuwa amefungua kesi hiyo namba 66 ya mwaka 2019 kuomba Mjane aondolewe na yeye kupewa jukumu hilo kwa madai ameshindwa kutimiza majukumu yake katika kugawa mali na akituhumu kuuzwa kwa baadhi ya mali.

Hata hivyo, mjane huyo kwa sasa yupo magereza akituhumiwa kwa kesi ya mauaji ya wifi yake Aneth Msuya ambaye aliuawa jijini Dar es Salaam.

Uamuzi wa kuondolewa shauri hilo ulitokana na maombi ya wakili wa Miriam na watoto wa Msuya.

“Upande wa Msuya wamefungua kesi hii mara ya tatu baada ya mbili kufutwa wakiomba kumuondoa msimamizi wa mirathi ambaye tayari alipitishwa na mahakama na wao kupokea mgao wa fedha zaidi ya Sh900 milioni,” alisema.

Hoja hiyo pia iliungwa mkono na mtoto mkubwa wa bilionea huyo, Kelvin Erasto ambaye amesema ndugu wa upande wa baba yake wanataka kuwapora mali kwa sababu pia ni mashahidi wa kesi ya mama yake

No comments: