Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisoma taarifa kwenye kikao kati ya Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe
Naibu Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro leo ameongoza ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye kikao kati ya Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje , Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Bunge jijini Dodoma. Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Musa Azzan Zungu (MB), kwa pamoja wameipongeza Wizara kwa kutekeleza vyema mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo katika vikao vilivyopita, sambamba na utekelezaji mzuri wa vipaumbele na malengo ya Wizara.
Kikao hicho kilitoa fursa kwa Wizara kuwasilisha kwa kamati taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu yake. Aidha, kikao hicho hutoa fursa kwa kamati kupokea na kujadili taarifa za Wizara pamoja na kutoa mapendekezo yake kuhusu masuala mbalimbali.
Kikao cha Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kikiendelea.
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia taarifa ya Wizara iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao.
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia taarifa ya Wizara iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Musa Azzan Zungu (MB), akichangia jambo wakati wa kikao.
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia kikao.
No comments:
Post a Comment