Diwani Nguvu Chengula akiongea kwenye mkutano wa kusikiliza kero kwa madereva bajaji na madereva boda boda wa Manispaa ya Iringa wakati wa kusikiliza kero zao mbele ya mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Umoja wa vijana wa chama cha
mapinduzi mkoa wa Iringa kimempongeza diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Edward
Chengula kwa mchango anaoutoa wa kusaidia kutatua baadhi ya changamoto ambazo
wamekuwa wanakumbana nazo.
Akizungumza kwenye mapokezi ya
mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Kenani Kihongosi mara baada ya kumaliza
majukumu ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa na kurudi kwenye majukumu ya
kichama mkoani Iringa,katibu wa UVCCM manispaa ya Iringa Sai Samba alisema kuwa diwani Nguvu Chengula
amekuwa akitoa misaada mbalimbali katika umoja huo.
“Ndugu mwenyekiti unaona vijana
hawa wa green guard wamependeza kwa sare safi,hivi zote ni juhudi za diwani
huyu ambaye alijitolea kitambaa ambacho kilisaidia kushona sare hizi japo bado
tunauhitaji wa sare hizo na bado amekuwa msaada wa kwenye mambo mengi ya umoja
wetu” alisema Samba
Samba aliongezea kuwa UVCCM
manispaa ya Iringa bado wanauhitaji mkubwa wa sare za green guard hivyo
wanaomba msaada kwa diwani huyo kuwawezesha kupata sare nyingine ambazo
zitawawezesha vijana wote wa green guard kuwa na sare ambazo zitatumika kwenye
matukio mbalimbali ya chama.
“Mheshimiwa diwani ikikupendeza
tunaomba tuongezee kitambaa kingine ili tushone sare ambazo zitakuwa zimetatua
tatizo hilo licha kuwa bado umoja huo unachangamoto nyingi” alisema Samba
Naye mwenyekiti wa umoja wa
vijana wilaya ya Iringa Vijijini Makalah Mapesa alisema kuwa moja kati ya
madiwani wa Iringa Mjini ambaye amekuwa na msaada katika wilaya hiyo ndi diwani
Nguvu Chengula ambaye amekuwa akisaidia mambo mengi
"kiukweli mimi naomba nimpongeze diwani Nguvu Chengula kwa mchango wake ambao amekuwa akiutoa wilaya ya Iringa vijijini kimaendeleo" alisema Mapesa
Kwa upande wake mwenyekiti wa
umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa (UVCCM) Kenani Kihongosi
alimpongeza diwani huyo kwa mchango wake kwa kuwa amepokea salamu kutoka kwa
viongozi wake wa chi kwa juhudi anazozifanya kuhakikisha anatatua changamoto za
umoja huo.
“Kama kweli unatoa msaaada huo
kwa roho nzuri mimi kama mwenyekiti nakupongeza sana ila kama unatoa kwa lengo
la kitu hapo baadae basi jiandae kukatwa jina pindi utakapoanza harakati zako
hivyo niwakumbushe viongozi wa CCM mkoa wa Iringa kuacha tabia ya kutoa Rushwa
kwa vijana” alisema Kihongosi
No comments:
Post a Comment