Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari wa mkoa Iringa juu ya hatma ya soko kuu la Mlandege lililopo katika manispaa ya Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi akimsikiliza kwa makini mkandarasi wa soko la kisasa la Mlandege Manispaa ya Iringa
Moja ya eneo la soko kuu la kisasa la Mlandege lilopo Manispaa ya Iringa
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally salumu hapi amefanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa soko kuu na la kisasa mlandege mjini Iringa na
kuagiza kasi ya ujenzi iongezwe na mkandarasi wa Home Africa Constractions Engineering
Ltd anayejenga soko hilo ili hadi kufikia October 31 mwaka huu liwe
limekamilika tayari kwa matumizi ya wafanyabiashara.
Katika Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama ya kutembelea na kukagua ujenzi wa soko jipya unaoendelea hivi sasa mjini Iringa Hapi alionesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo huku akitoa agizo la kuhakikisha linakamilika mwishoni mwa mwezi huu Mwaka Huu.
“Ndani ya tarehe 31 mwezi huu kumi taa zote,umaliziaji vitu vyote ya soko hili viwe vimekamilika,nataka ifikapo mwezi wa 11 tarehe 1 tayari muwe tayari kukabidhi mradi huu wa kisasa kwa halmashauri ili iweke utaratibu wa mzuri wa matumizi kwa hiyo nawapa siku saba tuu soko hili liwe imekamirika”alisema hapi.

Aidha Hapi alisema kuwa mradi
huo unagharimu shilingi bilioni 3.7 huku akimtaka mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa na wataalamu kuhakikisha wanaweka mpangilio
mzuri wa watu kupata vibanda na maduka kwa halali bila manung’uniko na waliokutwa
mwanzo ndio wapewe kipaumbele.
Alisema mkoa wa Iringa hauna
duka kubwa la kisasa la kuuza bidhaa ,hivyo halmashauri iangalie katika soko
hilo eneo wanaloweza kuweka kwajili ya uwekezaji wa duka kubwa litakalokuwa
linatoa bidhaa zenye ubora ili kuongeza pato la hamashauri.
“Naomba nitumie fursa
hii kuwapongeza sana mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela,mkurugenzi na
mkandarasi kwa kazi kubwa mliyoifanya kuhakikisha soko hili linakamili hivi
karibuni” alisema Hapi
Simon s. bahegwa ni
mkandarasi wa kampuni ya home Africa constractions alimesema kuwa thamani ya
mradi ilikuwa shilingi bilioni 3.72 na ifikapo tarehe 31 october watakuwa
wamekamilisha kama alivyoagiza mkuu wa mkoa.
“ mheshimiwa kufikia tarehe 31 mwezi huu tutakuwa tumekamilisha
mradi huu kwa asilimia 100 kwa tukimaanisha kufunga taa ,na thamani ya mradi
huu ilikuwa ni shilingi bilioni 3.72 na fedha iliyotumika mpaka sasa ni bilioni
2.6 tunategemea kukabidhi mradi huu
mwishoni mwa mwezi huu”alisema bahegwa
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya iringa HAMID NJOVU alisema kuwa soko hilo la Mlandege linaukubwa wa Squermeter 3182 ambapo wanatarajia likianza kutumika litakuwa likiingiza mapato ya shilingi million 55 mpaka milioni 80 kwa mwezi.
Mradi wa ujenzi wa soko jipya la Mlandege Manispaa ya Iringa unagharimu taklibani shilingi bilioni 3.7 kwa fedha za serikali unaotarajiwa kuwa na jumla ya wafanyabiashara 2000 .
No comments:
Post a Comment