Advertisements

Wednesday, January 8, 2020

Card B atangaza kuhamia Nigeria, kukimbia vita ya Iran na Marekani

Kama wazo la rapa Card B litaungwa mkono na wasanii wengi wa Marekani, tujiandae kuwapokea kwa wingi Afrika.

Rapa huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter leo Jumatano Januari 8, 2020 ameandika atalazimika kuchukua uraia wa Nigeria ili apate kwa kukimbilia.

Ameandika atachukua hatua hiyo kufuatia hofu ya kuwapo kwa vita ya tatu ya dunia inayotokana na Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kutokaa kimya mashambulizi yaliyofanywa na Iran katika kambi mbili za wanajeshi wa Marekani zilizopo nchini Iraq kushambuliwa kwa makombora kadhaa.

Runinga ya kitaifa ya Iran imetangaza shambulio hilo ni la kulipiza kisasi mauaji ya kamanda mkuu Qasem Soleimani aliyeuawa katika shambulio la ndege isiyokuwa na rubani mjini Baghdad, kufuatia agizo la Rais Trump.

Mshindi huyo wa tuzo ya Grammy ambaye jina lake kamili ni Belcalis Marlenis Almánzar amesema vita hiyo ikianza anahamia Nigeria na atamshawishi mume wake Offset kufanya hivyo.

Mwezi uliopita rapa huyo alifanya shoo nchini Nigeria na Ghana na inawezekana kwa siku alizoishi nchini humo ameona anaweza kuwa salama , kuliko kubaki Marekani iwapo kutakuwa na vita.

Masta wengine waliochukua uraia wa nchi mbili moja ikiwa ni Afrika ni pamoja na mwigizaji wa nchini Uingereza Idris Alba ambaye alichukua uraia wa Siera leone.

Mwigizaji na rapa Ludacris naye alichukua urai wa Gabon.

Mwananchi

No comments: