ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 9, 2020

CFAO Motors wazindua kizazi kipya cha Mercedes Benz

 Baadhi ya wageni waalikwa wakilitazama toleo jipya la kizazi cha tano cha Mercedes Benz – Actros Mirror Cam wakati wa hafla ya uzinduzi wa toleo hilo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.


 Mkurugenzi wa Mauzo wa CFAO Motors Tanzania Ltd, Bi. Tharaia Ahmed (katikati) akimkaribisha Mwakilishi wa Asas Group of Companies, Bw. Faraj Abril (kushoto) wakati wa kuwasili kwa wateja na wageni mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa toleo jipya la kizazi cha tano cha Mercedes Benz – Actros Mirror Cam uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Mauzo wa CFAO Motors Tanzania Ltd, Bi. Tharaia Ahmed akiendelea kupokea wageni waalikwa walipokuwa wakiwasili wakati wa hafla ya uzinduzi wa toleo jipya la kizazi cha tano cha Mercedes Benz – Actros Mirror Cam uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Huu ni muonekano wa jinsi Mirror Cam inavyoonekana kwa ndani karibu na usukani wa dereva wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa toleo jipya la kizazi cha tano cha Mercedes Benz – Actros Mirror Cam uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Mauzo wa CFAO Motors Tanzania Ltd, Bi. Tharaia Ahmed akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa toleo jipya la kizazi cha tano cha Mercedes Benz – Actros Mirror Cam uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Brandi ya Mercedes Benz wa kampuni ya CFAO Motors Tanzania Ltd, Bw. Jerome Sentimea akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa toleo jipya la kizazi cha tano cha Mercedes Benz – Actros Mirror Cam uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors Tanzania Ltd, Marius Prinsloo akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa pamoja na wateja wa kampuni hiyo (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa toleo jipya la kizazi cha tano cha Mercedes Benz – Actros Mirror Cam uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Brandi ya Mercedes Benz wa kampuni ya CFAO Motors Tanzania Ltd, Bw. Jerome Sentimea akizungumza kuhusu mifumo mipya ya kiteknolojia inayopatikana ndani ya toleo jipya la kizazi cha tano cha Mercedes Benz – Actros Mirror Cam wakati wa hafla ya uzinduzi wa malori hayo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wateja wa kampuni ya CFAO Motors Tanzania Ltd wakifurahi jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa toleo jipya la kizazi cha tano cha Mercedes Benz – Actros Mirror Cam uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors Tanzania Ltd, Marius Prinsloo (kulia) akimkabidhi mteja ambaye ni Mwakilishi wa Asas Group of Companies, Bw. Faraj Abril (katikati) mfano wa funguo ya toleo jipya la kizazi cha tano cha Mercedes Benz – Actros Mirror Cam. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa uzinduzi wa totelo hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. CFAO Motors Tanzania Ltd ndio wenye kibali cha biashara cha magari ya Mercedes Benz nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors Tanzania Ltd, Marius Prinsloo (kulia) akimkabidhi mteja Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Bhanji Transport, Bw. Rahim Bhanji (wa pili kulia) mfano wa funguo ya toleo jipya la kizazi cha tano cha Mercedes Benz – Actros Mirror Cam. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa uzinduzi wa totelo hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. CFAO Motors Tanzania Ltd ndio wenye kibali cha biashara cha magari ya Mercedes Benz nchini. Anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja wa Brandi ya Mercedes Benz, Bw. Jerome Sentimea (kushoto) .

Na Mwandishi wetu
MALORI ya Mercedes Benz kizazi cha tano yenye mifumo mipya na muonekano bora kabisa yameingia nchini na kampuni ya CFAO Motors Tanzania Ltd ambao wana kibali cha biashara cha malori hayo imeyazindua mwishoni mwa wiki.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors Tanzania Ltd, Marius Prinsloo alishukuru wateja wa Mercedes Benz kwa kuendelea kuwa na imani na malori hayo.
Alisema kutokana na tayari kuna oda za uniti 40 za malori yenye mfumo mpya ambao ni salama na unaojali maslahi ya dreva na mmliki wake.
Toleo hilo jipya Mercedes Benz – Actros Mirror Cam ni kizazi cha tano kikiwa na mifumo mipya ndani ya gari kuwezesha kupiga mwendo zaidi kwa usalama na kujiamini.
Aidha alisema kwamba biashara ya malori hayo inazidi kukua nchini na kutokana na sababu hiyo wamejinyakulia tuzo ambayo imewajengea heshima kama wawakilishiwa Mercedes Benz nchini.
Alisema mauzo ya magari hayo ya Mercedes Benz yameendelea kukua nchini kutokana na ubora wake na pia huduma ya CFAO kabla na baada ya mauzo ya malori hayo.
Naye meneja wa Brandi ya Mercedes Benz wa CFAO Motors Tanzania Ltd, Jerome Sentimea amesema pamoja na muonekano bomba wa malori hayo, vioo vyake vya nje (side Mirror) kwa sasa vipo ndani vikiona kila kitu kupitia kamera ndogo zilizowekwa katika gari hilo.
Pia gari hilo jipya lina mifumo ya sensa kiasi ya kwamba kama kuna kituo chochote kinakatisha mbele hata kama uko katika spidi ya namna gani, linajisimamisha lenyewe.
Anasema malori hayo mapya ya kizazi cha tano yametengenezwa pia kumwezesha dereva wake kuongea na simu bila kushika simu kwa maana mfumo unamwezesha kupachika simu yake ambayo itaunganishwa na spika za katika gari.
"Simu ikiita hata kama dereva alikuwa na anasikiliza muziki  ule muziki utakatika na yeye kusikiliza simu yake bila kuishika" alisema Sentimea.
Pia magari hayo mapya yametengenezwa kwa ajili ya mataifa ya Afrika kwa kunyanyuliwa (Ground clearing) kiasi ya kwamba haiwezi kugonga  chini hata kwenye barabara mbaya.
Sentimea alisema tayari wamepata oda ya magari 40 ya aina hiyo kutokana na wasafirishaji kuona yanakidhi vigezo vya wasafirishaji hasa usalama wa chombo.
Alisema kizazi cha sasa kimezingatia ukweli kuwa magari mengi yakirudi safari yalikuwa hayana side mirror  na katika ulimwengu wa teknolojia yalikuwa yanamfanya dereva asiwe salama wakati wa kupokea simu yake.
Pia amesifu kuwa matumizi ya mafuta katika kizazi cha tano ni mazuri zaidi kwa kuwa vikinga upepo (Side mirror ) vimeondolewa.
Camera zilizowekwa zinasaidia dereva kuona ukubwa wa gari lake na pia kujua umbali halisi bila kutazama kioo cha nje, hivyo kumuongezea uwezo zaidi wa kulitambua gari bila kujiumiza na kujichosha.
Pamoja na usalama wa gari dereva pia akisimama anaweza kujua usalama wake kabla ya kushuka kupitia mifumo mipya.
Rahim Bhanji, Mkurugenzi wa taasisi ya usafirishaji ya Bhanji amesema kwamba ameamua kununua malori hayo kutokana sifa zake zinazomhakikishia upunguzaji wa gharama.
Alisema kutokana na maelezo ya ufanisi anaona kwamba gari hilo lina tija.

No comments: