ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 10, 2020

TAARIFA MUHIMU, TUZO ZA TEHAMA ZA TCRA, 2020, (TCRA ICT AWARDS, 2020)

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini wakati wa kikao kazi.

Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu ya jamii
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mhandisi James Kilaba amesema kwa mamlaka hiyo iko kwenye mchakato wa kutoa tuzo za TEHAMA kwa wadau wao wenye leseni za TCRA na kwamba tuzo hizo zimepewa jina la TCRA ICT Award 2020 huku akitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa vyombo vya habari nchini kushiriki kikamilifu kufanikisha mchakato huo.

Mhandisi Kilaba ameyasema hayo leo kwenye ufunguzi wa kikao kazi na wahariri pamoja na waandishi waandamizi kilichofanyika leo Machi 5 mwaka 2020 jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza wazi kuitikia mwito wa Mamlaka hiyo wa kuhudhuria kikao hicho maalum.cha kazi kutaleta manufaa makubwa kwa wadau na Taifa kwa ujumla.

"Kama mnavyofahamu TCRA iko kwenye mchakato wa kutoa tuzo za TEHAMA kwa wadau wetu wenye leseni, tuzo ambazo zimepewa jina la TCRA ICT Awards 2020.Najua miongoni mwetu au Taasisi zenu zina leseni za TCRA na hivyo mashariki kikamilifu katika mchakato huu,"amesema .

Mhandisi Kilaba ameongeza kama walivyowashirikisha awali,mchakato huo ulizinduliwa Januari 31 mwaka huu wa 2020 katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wahariri na waandishi waandamizi waliokuwepo.

"Katika uzinduzi ule TCRA ilitoa idadi ya makundi ya washiriki ambayo yaliwekwa kwenye tovuti maalum ya Mamlaka ili wadau wote muweze kujua makundi yanayoshiriki kwenye mchakato huu.TCRA pia alisisitiza ulazima wa wenye leseni za TCRA wote kushiriki.Kwa taarifa ambazo tumekuwa tunawashirikisha ,sasa tunaelekea mwisho wa uwasalishaji wa nia ya kushiriki kwenye shindano hili ni Machi 15 mwaka huu,"amesema.

Ameongeza baada ya hapo awamu ya mchakato huo utaanza Machi 16 mwaka huu ambapo itatoa fursa kwa wananchi kushiriki kupiga kura kwa mtoa huduma bora kwa utaratibu ulioandaliwa.Katika awamu hiyo ushiriki wa wahariri na Waandishi ni muhimu katika kuhabarisha Umma ili uweze kushiriki kikamilifu katika mchakato huo.

Mhandisi Kilaba amesema tangu mchakato huo uanze wamepata ushirikiano mkubwa kutoka vyombo vya habari ingawa bado TCRA inaamini ushiriki wa vyombo hivyo ungeweza kuwa mkubwa zaidi na kwamba kukutana kwao leo kunalenga kuweka mikakati ya pamoja ya jinsi ya kuboresha ushiriki wa vyombo vya habari kwenye mchakato huo.

"Kuna mambo ambayo tungependa kushirikiana zaidi na hii inatokana na utashi wetu ambao umo katika mkataba wetu wa huduma kwa mteja Ninaamini Webb wetu tumeusoma mkataba huu.Mkataba huu unakusudia kuimarisha utamaduni wa utendaji bora unaozingatia mahitaji, matakwa na matarajio ya wateja na wananchi kwa ujumla,"amesema.

Mhandisi Kilaba amesema yeye binafsi kinathamini nguvu ya vyombo vya habari katika kuelimisha na kuhabarisha Umma.Hatua waliyofikia katika utaratibu huo wa Tuzo za TEHAMA unahitaji uhamasishaji wenu na kuhimiza kila mmoja wao ashiriki lakini kuelimisha wengine kushiriki na kwamba ufanisi wa tuzo hizo utategemea na wingi wa washiriki.

Amefafanua kwasababu tuzo hiyo ni ya kwanza kuandaliwa katika nchi yetu, wadau na wananchi wengine wakafikiria kwamba jambo hilo si kubwa au hakuna thamani.Pengine kupitia kikao hicho ameamua kukumbusha umuhimu wa tukio hilo.

Amesema ni vema kuwatambua na kuwatunuku watoaji wa huduma Bora zaidi za Mawasiliano, kuongeza ubunifu katika utoaji wa huduma za utangazaji, kuongeza ubora na ufanisi wa huduma za Mawasiliano katika sekta za posta, simu,utangazaji na intanet pamoja na kuongeza chachu na mchango wa sekta ya nawasiliano katika kukuza uchumi wa kidijitali.

No comments: