Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya kuandaa taarifa ya Kitaifa ya Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni, Bw. Boniface Kadili (kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya kuandaa rasimu hiyo Robert Mwampemba pamoja na Mkufunzi kutoka Unesco, Bw. David Waweru wakati wakimsubiri mgeni rasmi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kuwasili kwenye halfa ya kupokea na kuridhia taarifa ya kitaifa ya Mkataba wa Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya kuandaa taarifa ya Kitaifa ya Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni, Bw. Robert Mwampemba, Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-Unesco), Profesa Hamisi Malebo, Bw. Joel Samwel, Mkurugenzi kutoka Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Emmanuel Temu, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe pamoja Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Nancy Kaizilege.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe pamoja na washiriki (hawapo pichani) wakati halfa ya kupokea na kuridhia taarifa ya kitaifa ya Mkataba wa Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Nancy Kaizilege akitoa salamu kwa niaba ya UNESCO wakati halfa ya kupokea na kuridhia taarifa ya kitaifa ya Mkataba wa Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-Unesco), Profesa Hamisi Malebo, Bw. Joel Samwel akitoa salamu za NATCOM wakati halfa ya kupokea na kuridhia taarifa ya kitaifa ya Mkataba wa Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya kuandaa taarifa ya Kitaifa ya Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni, Bw. Boniface Kadili akitoa muhtasari wa taarifa ya Kitaifa ya Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni wakati halfa ya kupokea na kuridhia taarifa hiyo kwa Waziri Mwakyembe iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya kuandaa taarifa ya Kitaifa ya Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni, Bw. Robert Mwampemba akielezea muhtasari wa ripoti hiyo kwa wadau mbalimbali wakati halfa ya kupokea na kuridhia taarifa hiyo kwa Serikali iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Nancy Kaizilege wakati halfa ya kupokea na kuridhia taarifa hiyo kwa Serikali iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akimkabidhi cheti mjumbe wa kamati ya kuandaa taarifa ya Kitaifa ya Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni ambaye pia ni Meneja Miradi wa CDEA, Bw. Mandolin Kahindi wakati wa halfa ya kupokea na kuridhia taarifa hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni kushoto Mkurugenzi kutoka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Emmanuel Temu na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Bi.Nancy Kaizilege aliyemwakilisha Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akimkabidhi cheti mjumbe wa kamati ya kuandaa taarifa ya Kitaifa ya Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni kutoka visiwani Zanzibar Bi. Saumu Ali wakati wa halfa ya kupokea na kuridhia taarifa hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni kushoto Mkurugenzi kutoka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Emmanuel Temu na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO nchini, Bi.Nancy Kaizilege aliyemwakilisha Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Tirso Dos Santos.
Baadhi ya wadau kutoka katika tasnia mbalimbali nchini walishiriki wakati wa halfa ya kupokea na kuridhia taarifa ya Kitaifa ya Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni kwa Serikali iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati iliyoandaa taarifa ya Kitaifa ya Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni wakati wa hafla ya kupokea na kuridhia taarifa hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
TATIZO la Watanzania kushindwa kuziwahi fursa duniani, kunafanya mataifa mengine kuwahi kuzitumia fursa ambazo watanzania ndio wangeliweza kuzichukua na kufaidika nazo.
Aidha imeelezwa kuwa kutokana na tatizo hilo upo uwezekano mkubwa duniani wa Kiswahili ambacho ni fursa kwa watanzania kusambazwa na taifa la China kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na taifa hilo.
Kauli hizo zimetolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni, Dk Harrison Mwakyembe wakati akizindua taarifa ya kitaifa ya Mkataba wa Kulindwa, Kuendelezwa Uanuai wa Kujieleza Kiutamaduni
Alisema pamoja na kuzindua taarifa hiyo ambayo itasomwa duniani na hivyo kutoa fursa kwa watanzania alisema imekuwa ni kawaida kwa Watanzania kuwa taratibu sana katika kukimbilia fursa mbalimbali.
Alisema kuwepo kwa taarifa hiyo kunamaanisha kwamba sasa dunia itajua Tanzania kuna nini na wanaweza kufanya nini, hali ambayo inawataka wananchi kujiandaa kupokea fursa mbalimbali kutoka ndani na nje inayohusu masuala ya sanaa na ubunifu.
“Tuna tatizo la kushindwa kuwahi fursa zinazojitokeza.. mfano Kiswahili, fursa zipo kila sehemu lakini watanzania wanaojitokeza ni wachache” alisema na kuongeza kuwa ikiwa miongoni mwa lugha 10 katika lugha 6000 duniani zinazofanya vyema, Watanzania wanashindwa kutumia lugha hiyo kama fursa kufundisha wengine.
Alisema wameanzisha kanzidata kutokana na mahitaji makubwa ya walimu wa kiswhaili duniani, lakini mpaka sasa kuna watanzania 1,500 waliojisajili kati ya wanafunzi zaidi ya 20,000 waliojifunza Kiswahili katika vyuo vya Tanzania.
Alisema wakati watanzania bado wanasuasua wanapata majina ya watu wanaotaka kuorodheshwa katika kanzidata hiyo kutoka mataifa mengine yakiwemo Kenya na Uganda.
Alisema kwamba China kwa sasa inatoa wahitimu wengi wa Kiswahili na wanaingia katika sekta kwa kasi kuliko Watanzania wanavyofanya.
“Leo hii ukimshauri mtoto kusomea public relations au international relations unamkosesha ajira, ajira ipo kwenye Kiswahili” alisema.
Akihutubia kikao cha kujadiliana rasmi cha kitaifa kwa mujibu wa taratibu za UNESCO ambao ndio wafuatiliaji wa mkataba huo alisema Mkataba huo ambao uliridhiwa nchini mwaka 2011 ulitiwa saini mwaka 2005 na una malengo manne yakiwemo uhuru wa kujieleza kiutamaduni na kuwapo na fursa na haki katika sekta ya ubunifu na sanaa.
Ikifafanuliwa zaidi imeelezwa kuwa malengo manne ya mkataba huo ni pamoja na kuangalia mifumo mizuri ya utawala katika utamaduni, masuala yanayohusu mauzo ya sanaa na wasanii wenyewe, Uingilianaji wa shughuli za sanaa na mipango ya taifa na kuimarisha haki za binadamu.
Alisema ni vyema watanzania wakaijua tunu iliyoachwa na mwalimu Nyerere ya Kiswahili ambayo ikitumika vyema itasaidia sio kutengeneza ajira bali kuwa na nafasi huru ya kujieleza kitamaduni.
Alisema wakoloni walitumia hila kutumbukiza mambo yao na kuvunja utamaduni wetu ili waweze kututawala na ingawa tuliamka kupitia mapinduzi ya uafrika Marekani kwenye miaka ya 1960 kwa sasa wamefanikiwa kutokana na kushawishi matumizi ya dawa kubadili nywele na pia muonekanao wa mwili.
Alisema lengo la wakoloni ni sisi kujidharau wenyewe ili wapate nafasi ya kututawala lakini tukiacha kujidharau na kushikilia yaliyoyetu tutajinasua na mikono yao.
Pamoja na kuingia katika ulimwengu wa kidigitali alitaka vijana kutambua yaliyojiri jana ili waweze kuwa na nafasi kubwa ya kujiamini na kujitawala.
Aidha alisema taarifa hiyo inayopelekwa katika ’portal’ ya Unesco itasaidia pia kwa serikali kujitathmini na kujua nini kinatakiwa kufanyika hasa katika masuala ya sera na pia namna ya kuwafanya wabunifu mbalimbali kuneemeka na shughuli wanazofanya.
Alisema serikali inathamini mchango wa ubunifu maendeleo ya taifa na kusema sekta ya utamaduni sasa inazidi kuongoza kwa kukua hata katika bajeti.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya kuandaa rasimu hiyo Robert Mwampemba alisema kwamba rasimu hiyo imeibua mambo mengi lakini kikubwa imesaidia taifa kutambulika kimataifa na mipangilio iliyopo nchini kuhusu utamaduni na sera zake.
Taarifa hii imeandaliwa na Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM) Ofisi ya UNESCO kanda ya Afrika Mashariki, UNESCO Dar chini ya ufadhili wa Sweden kupitia Mfuko wake wa Maendeleo (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO Dar.
No comments:
Post a Comment