ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 28, 2020

Bariadi wapewa mashine za kusaidia wenye corona kupumua


Derick Milton, Simiyu, Mtanzania

Uongozi wa Kituo cha Afya cha Songambele kilichopo katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu umetoa mashine nne kwa ajili ya kusaidia watu wenye maambukizi ya virusi vya corona ambao watakuwa na tatizo la kupumua.

Kituo hicho ambacho kinamilikiwa na mtu binafsi kimetoa msaada huo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo ambapo wenye matatizo hayo wataweza kupata huduma hiyo bure kituoni hapo.

Mashine hizo ambazo zimefungwa katika kituo hicho, zitatumiwa bure endapo mgonjwa wa corona atagundulika kuwa na tatitizo la kupumua katika kipindi chote cha mapambano ya ugonjwa huo.

Akiongea mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Stephano Mabula amesema kuwa mgonjwa yoyote ambaye atagundulika kuwa ameambukizwa Corona na ana atatizo la kupumua mashine hizo zitumike kumsaidia bure.

Mbali na kituo hicho, Jumuiya ya Wafanyabishara wa wilaya hiyo kwa kushirikiana na Mbunge wa jimbo, Adrew Chenge wametoa kiasi cha Sh. milioni 3.9 kwa ajili ya kununua vifaa vya kujikinga na ugonjwa huo.

No comments: