ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 28, 2020

UBALOZI WA KENYA NCHINI UINGEREZA WATANGAZA TAREHE MPYA YA KUWARUDISHA WAKENYA NYUMBANI

Ubalozi wa Kenya nchini Uingereza umetaja tarehe mpya ya kuwarudisha nyumbani waKenya waliokwama nchini Uingereza kutokana na usafiri wa anga kusitishwa kwa muda kutokana na janga la Corona.

Tarehe iliyokua imetangwazwa hapo awali ilikua ni April 25, 2020 ambapo shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways lilikua limepanga kuwachukua waKenya waliokua wamekwama nchini Uingereza kutokana na safari za anga kusitishwa kwa muda.

Ubalozi wa Kenya nchini Uingereza umetangaza tarehe mpya itakua May 4, 2020. Balozi wa Kenya nchini Uingereza Mhe. Manoah Esipisu amesema sasa ndege ya Kenya Airways itaondokea uwanja wa ndege wa kmataifa wa Heathrow uliopo jiji la London siku ya Jumatatu.

Wakenya waliokwama nchini Uingereza wametakiwa kukata tiketi moja kwa moja kupitia shirika hilo la ndege la Kenya Airways na kuruhusiwa kusafiri Balozi Esipisu amesema wasafiri wote lazima waonyeshe cheti kwamba hawana maambukizi ya Corona.

No comments: