ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 28, 2020

Tanzania: Waliothibitika Kuwa na Corona Wafikia 306

WIZARA ya Afya Zanzibar imetoa taarifa ya ongezeko la wagonjwa wapya saba walioambukizwa virusi vya corona na kufikisha idadi ya wagonjwa 105 kutoka 98 visiwani humo. Wagonjwa wote wapya ni raia wa Tanzania na wametokea visiwani Unguja. Kwa ongezeko hili sasa idadi ya visa vya corona Tanzania nzima imefikia 306 kutoka 299 tangu ugonjwa huo uingie nchini.

“Wagonjwa wote ni Watanzania, wametoka Unguja, jumla ya wagonjwa 36 wameruhusiwa kwenda nyumbani wanashauriwa kubaki ndani ya nyumba zao siku 14, huku wataalamu wa Afya wakiendelea kuwafuatilia,” amesema Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid.

Serikali imetoa wito kwa wananchi kuendeea kuchukua tahadhari. Pia kwa wenye dalili wametakiwa kupiga simu namba 190. Aidha, wizara imevitaka vyombo vya habari kupata taarifa za virusi vya Corona kutoka kwa Wizara ya Afya 
GPL

No comments: