Friday, April 17, 2020

BARUA KUTOKA WA BALOZI MASILINGI KWENDA KWA MWENYEKITI WA BODI DICOTA

Kikwete appoints Masilingi new ambassador to USA - The Citizen
Mhe. Wilson Masilingi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi  amesema michango inayoratibiwa na DICOTA katika kuchangangisha waTanzania nchi Marekani, Ubalozi hauusiki kwa namna yeyote vile hilo ni wazo la DICOTA wenyewe.

Mhe. Balozi Masilingi amesema hayo leo baada ya kuona ujumbe wa kuchangisha fedha za kusaidia wahanga wa COVID-19 nchi Tanzania ukisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ukitaja jina la Ubalozi.

Katika ujumbe huo unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Marekani umetaja umepata baraka kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kitu ambacho Balozi Mhe. Wilson Masilingi amepingana nacho, Nahii hapo chini ni barua pepe aliyomwandia Mwenyekiki wabodi ya DICOTA Bi. Asha Nyng'anyi.

Bi Asha Nyanganyi,
Mwenyekiti wa Bodi,
DICOTA.

Salaam.

Nasikitika siwezi kutekeleza maombi yenu ya kuwapatia ninyi DICOTA barua ya Ubalozi kuwasaidia kuchangisha pesa taslimu kutoka kwa DIASPORA Watanzania waishio Marekani, Wamarekani wenye asili ya Tanzania au Marafiki wa Tanzania. Rejea tahadhari niliyowapa kuhusu kuchangisha pesa taslimu au mchango wowote toka Diaspora au marafiki wa Tanzania katika barua pepe yangu ya Aprili 6, 2020 nikijibu barua pepe kutoka kwenu. 

Watanzania wenzetu waliowengi waishio hapa Marekani wanapitia katika kipindi kigumu baada ya shambulio la COVID-19. Baadhi ya Watanzania wenzetu hapa hapa Marekani wameugua ugonjwa huo hatari COVID-19 na wengine bado wamelazwa katika Majimbo mbali mbali. Tunawaombea Mwenyezi Mungu awaponye haraka. Aidha Watanzania wengi kama ilivyo kwa Wenyeji wetu Wamarekani wanahangaika kupata chakula baada ya kufungwa kwa shughuli za Kiuchumi! Ubalozi ambao nimepewa upendeleo na heshima kuongoza, kipaumbele kikiwa ni kulinda na kutetea uhai na maslahi ya Watanzania, kwa bahati mbaya Ubalozi wetu hauna uwezo wa kuwapa msaada wa chakula wala fedha.

Kwa upande wa Wamarekani wenye asili ya Tanzania waliopoteza ajira au biashara, kama unavyojua, Serikali yao inawapa misaada.

Narejea ushauri wangu kwenu, DICOTA ikiwa ni mojawapo ya Taasisi nyingi binafsi za Watanzania zilizosajiliwa Kisheria hapa Marekani, kwa ridhaa yenu, kwa ushawishi wenu, na kwa kuaminiwa kwenu na mtakao wachangisha fedha taslimu au chochote bila kutweza utu na heshima ya nchi yetu, Ubalozi wenu hauwezi kuwazuia kuchangia nchi yetu. Naomba nieleweke, Ubalozi hauchangishi pesa yoyote. Nisaidie kufikisha ujumbe huu. Kwa hiyo Ubalozi hatutawajibika kwa lolote kuhusu michango hiyo mtakayofanikisha.

Nawatakia mafanikio na ulinzi wa Mwenyezi Mungu katika kipindi hiki kigumu cha shambulizi la COVID-19.

Balozi Wilson M. Masilingi.

No comments: