Wednesday, April 15, 2020

IGP: Ukimamatwa Hujavaa Barakoa, Jela Miezi 6








MKUU wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, IGP Hilary Mutyambai amewaagiza polisi kumkamata mtu yoyote atakayeonekana mitaani bila kuwa na barakoa.
Kuvaa barakoa nchini humo ni lazima ili kuzuia maambukizi ya #Covid19. Suala hilo limeshatangazwa na gazeti la serikali kupitia ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali tangu Aprili 6, mwaka huu.

Kwa mujibu wa tangazo la gazeti hilo, kosa la kutovaa barakoa linaweza kupelekea faini ya KSh 20,000 sawa na takribani Tsh milioni 4.72 au kifungo cha miezi sita, au vyote kwa pamoja.\
Pia, tangazo limezitaka wafanyabiashara kuweka sabuni na maji kwa ajili ya wateja wao au vitakasa mikono vilivyothibitishwa na shirika la viwango vya Kenya.


Pia wafanyabiashara wametakiwa kuhakikisha wateja wanaachiana nafasi isiyopungua mita moja. Wafanyabiashara watakaokiuka tangazo hilo watalipa faini ya Tsh milioni 4.72 au kifungo cha miezi sita jela au vyote. Wizara ya afya pia imewataka bodaboda kubeba abiria mmoja tu kwa safari.

GPL 

No comments: