Wednesday, April 15, 2020

WATEJA SOKO LA KIHESA WAKAIDI AGIZO LA KUTAKASA MIKONO

 Kaimu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Joseph Ryata akiwa katika soko la Ipogolo alipofanya Ziara katika masoko ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kujua namna gani wafanyabisha wanaelimu ya kupambana na Virusi vya Corona
  Kaimu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Joseph Ryata akiwa katika soko la Mlandege alipofanya Ziara katika masoko ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kujua namna gani wafanyabisha wanaelimu ya kupambana na Virusi vya Corona
  Kaimu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Joseph Ryata akiwa katika soko la Ipogolo alipofanya Ziara katika masoko ya manispaa ya Iringa kwa lengo la kujua namna gani wafanyabisha wanaelimu ya kupambana na Virusi vya Corona

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.
WAFANYABIASHA soko la Kihesa Manispaa ya Iringa wameomba kuwepo na Askari wa Jeshi la akiba katika maeneo ya masoko ili kuwakamata wateja wanaokaidi kwa makusudi agizo la kutakasa mikono ili kujikinga na virusi vya Corona.
Akizungumza mbele ya kaimu meya wa Manispaa ya Iringa na wataalamu wa afya waliotembelea sokoni hapo Mwenyekiti wa soko hilo Subira Mohamedi amesema baadhi ya wateja wanakataa kutumia vitakasa mikono na kuzua hofu ya maambukizi.
Kaimu Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Ryata alisema Halmashauri haitosita kuchukua hatua za kisheria ikiwamo kuwafungulia mashtaka, watakaokaidi maagizo ya Wataalamu wa Afya yanayolenga kukabiliana na maambikizi ya corona
“Nimesikitishwa na kitendo cha wananchi kukataa kunawa mikono kwa sababu hiyo serikali itawachukulia hatua za kisheria kukabiriana na wananchi wanaogoma kutakasa mikono” alisema Ryata
Akiwa katika ziara maalam ya ukaguzi wa mwenendo wa mapamabano ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona katika masoko ya manispaa ya Iringa Kaimu Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Nzala Ryata alitembelea soko la kuu jipya la Mlandege,soko la ipogolo na soko la Kihesa, alisema kuwa bado kuna haja kubwa ya kuwaelimisha wananchi juu ya namna bora zaidi ya kujikinga na maambukizi ya corona.
“Bado kunatatizo kubwa na wananchi kutokuwa na elimu ya kupambana na virusi vya Corona katika Manispaa ya Iringa,hivyo kunahaja ya kutoa elimu endelevu ili wananchi watambue madhara yanayotokana na virusi hivyo” alisema Ryata
Ryata alisema bado kuna mikusanyiko mikubwa isiozingatia umbali unaotakiwa na wataalamu wa afya wamesema ni miongoni mwa changamoto yenye hatari kubwa pindi maambukizi yanapoibuka.
Hata hivyo hali ni tofauti kabisa katika Soko la Kihesa ambalo wamefanikiwa kuweka maji na sabuni maeneo yote ya kuingia na kutoka sokoni hapo pamoja na maeneo ya ziada wakiwa na lengo mahususi la kujikinga wao wenyewe
 Lakini changamoto inayoibuka ni baadhi ya wateja kukataa kutakasa mikono yao kutokana na wananchi wengi bado hawana elimu ya kujikinga na virusi vya Corona.
Kwa Upande wake afisa Afya John Bwire alisema wananchi wote watakaokaidi kutakasa mikono yao watakabiliwa na adhabu kali kwa mujibu wa kisheria za nchi
Aidha katika Ziara hiyo Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Jesca Leba alisema wanaendelea na mkakati wa kutoa tahadhari na elimu katika maeneo yote ya mikusanyiko

No comments: