ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 28, 2020

MWANAMKE WAKO AMEKUWEKA KUNDI GANI?

KATIKA mapenzi kuna mambo mengine yanaumiza lakini ni vizuri kujifunza. Ukijua inakuwa rahisi kukaa nayo mbali.

Kuna kitu nataka kukupa rafiki yangu mpendwa.
Je, unajua kuwa baadhi ya wanawake huwaweka wanaume katika makundi? Ndugu zangu baadhi ya wanawake wasio waaminifu wenye wanaume zaidi ya mmoja huwaweka wanaume kwenye makundi matatu.
Unaweza kuwa na msichana mkapendana sana, kwa sababu ya upofu wa mapenzi usijue amekuweka kundi lipi. Ni vizuri kuyafahamu makundi hayo kisha kujichunguza ili ujue kundi ulilopo.

MAKUNDI

Makundi hayo ni starehe, kutoshelezwa kimapenzi na fedha. Lazima uwe makini sana ili uweze kujua tabia za makundi hayo.
Inahitajika utulivu na umakini wa hali ya juu maana wakati mwingine, mwanamke anaweza kuonyesha dalili ya wazi ya kundi fulani lakini kutokana na kupumbazwa na mapenzi ukaamini kwamba umefika kwenye kiota cha raha za wapendanao.

KUNDI A

Unaweza kuwa kwenye kundi la starehe. Mwanamke akawa na wewe kwa lengo la kuwa na uhakika wa kupata starehe kila wiki. Hebu angalia tabia za mpenzi wako, yukoje?
Haina maana kwamba mwanamke akipenda starehe ni tatizo, lakini ukiona mazungumzo yake yanaonekana kujali zaidi starehe kuliko mambo mengine muhimu, ujue hapo upo kwenye mikono isiyo salama.
Mwanamke mwenye upendo wa dhati hawezi kuendekeza starehe, sana sana atakusubiri umshinikize mtoke.

KUNDI B
Wapo wanawake ambao wapo na wanaume kwa ajili ya kujipajia fedha. Fikra zao zote ni kupata fedha na siyo kitu kingine chochote. Atafanya kila kitu, atatafuta kila sababu lakini lengo lake ni kukuchuma.
Wanawake hawa wapo wa aina mbili, wengine huchuna fedha na kwenda kula raha na wanaume wengine huku wengine wakiwa ni wachumi kwa manufaa yao wenyewe.
Wachumi mara nyingi huwa na wanaume wengi wakiwa na lengo la kujipatia fedha. Ni kama wanajiuza lakini hawapo sokoni rasmi. Mwanamke wako yukoje?

KUNDI C

Kundi la mwisho ni lile la wanawake wanataka wanaume wa kuwatumia kimapenzi tu. Huyu hata usipompa fedha, shida yake kubwa huwa ni faragha.
Mara nyingi mwanamke wa aina hii anaweza kuwa mkubwa kiumri kuliko mwanaume lakini wakati mwingine anaweza kuwa na umri wa kati, sawa au chini ya mwanaume lakini haonyeshi nia ya malengo ya ndoa siku zijazo.
Huyu ni rahisi kumgundua hata katika mawasiliano tu. Anaweza kukuambia waziwazi anakutaka faragha, tena mara kwa mara. Hazungumzii maendeleo, hataki kujua habari zako, anachotaka ni mapenzi tu.

Asilimia kubwa ya wanawake wa namna hii ni wale ambao wana wenzi wengine wenye malengo nao lakini hawawatimizi haja zao za kimapenzi. Ni vizuri kuwa makini, kuchunguza na kupata uhakika kisha kuchukua hatua.

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Saikolojia ya Uhusiano anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Kwa sasa anaandaa kitabu chake kipya cha Maisha ya Ndoa
.

No comments: