Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hapo awali ni kwamba, ligib hiyo inatarajia kurejea tena Mei 16, lakini taarifa ya mambukizi hayo mapya kwa wafanyakazi wa Koln wakiwemo na wachezaji imezua maswali mengi, juu ya kurudishwa kwake.
"Tulichojifunza kutokana na janga hili ni kwamba, imetusaidia kupata kujua nani ana maambukizi na nani hana," alisema msemaji mkuu wa Bundesliga.
"Tunalichukulia jambo hili kwenye mlengo chanya na kamwe hatukati tamaa na kusitisha nia yetu ya kurejesha Ligi kati kati ya mwezi huu. Pia hatuna shaka kwani hao ambao wamekutwa na maambukizi hayo tayari wameshawekwa chini ya uangalizi kwa matibabu zaidi," alisisitiza.
"Tulifanya vipimo kwa siku chache zilizopita, hii yote ni katika kuhakikisha wale wote ambao watakuwa wanacheza basi wawe na afya njema," akliongeza msemaji huyo.
Lakini kwa upande wa kiongozi Ligi zote za Ujerumani, Tim Meyer alisema, wamejaribu kulifanyia kazi suala hilo la Ligi kuchezwa tena, na kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuishawishi Kamati ya Afya nchini humo na wamewapa baraka zote, kutokana na mikakati waliyowaeleza juu ya watakavyo hakikisha usalama wa wachezaji watakapokuwa dimbani.
"Tulijaribu kuwashawishi watu wa Afya kupitia mpango wetu ambao utawafanya wachezaji wacheze kwa uangalizi wa hali ya juu sana, na uhakika kwamba hakutakuwa na hatari" alisema Meyer.
Mpaka kufikia jana jioni klabu ya FC Koln, ilikuwa klabu pekee ya Bundesliga, wafanyakazi wake na wachezaji, kukutwa na maambukizi ya virusi hivyo, kabla ya hapo hakukuwa na timu iliyokutwa na kadhia hiyo.
Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment