ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 6, 2020

Tanzia: Sheikh Kilemile Afariki Dunia

MWANZUONI nguli wa Tanzania na Afrika Mashariki, Sheikh Suleiman Amran Kilemile, amefariki usiku wa kuamkia leo, May 06, 2020, katika Hospitali ya Sinza Dar es Salaam kutokana na matatizo ya kisukari.

Taratibu za mazishi zinaendelea leo hii katika Masjid Thaqafa-Tandika jijini Dar es Salaam, ili kuuandaa mwili kwa ajili ya kuzikwa.

Sheikh Kilemile alikuwa ni miongoni mwa masheikh nguli na wenye elimu kubwa katika uwanja wa elimu ya Kiislamu na Da’awah si tu Tanzania, bali Afrika Mashariki na ulimwengu mzima wa Kiislamu kwa kuwa alikuwa mahiri katika kila fani miongoni mwa fani za Kiislamu.

Ameandika na kutafsiri vitabu kadhaa na kuzalisha wanafunzi mahiri wengi na ni mmoja wa masheikh wachache waliotoa darasa muda mrefu katika Msikiti wa Chihota – Tandika miaka ya 80. GPL

No comments: