ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 5, 2020

Ummy Mwalimu aunda kamati kuchunguza upimaji sampuli za corona


Mwandishi Wetu, Dar es Salaam, Mtanzania

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameunda kamati ya wataalamu wabobezi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa mwenendo wa Maabara ya Taifa ya Afya ikiwamo mfumo mzima wa ukusanyaji na upimaji wa sampuli za corona.

Aidha, amemwelekeza Katibu Mkuu (Afya), kuwasimamisha kazi mara moja Mkurugenzi wa maabara hiyo, Dk. Nyambura Moremi na Meneja Udhibiti wa Ubora, Jacob Lusekelo ili kupisha uchunguzi.

Waziri Ummy amechukua hatua hiyo ikiwa ni utekelezaji wa changamoto zilizobainishwa na Rais John Magufuli jana Jumapili Mei 3, wilayani Chato alipokuwa akimwapisha Waziri wa Katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, katika maabara hiyo.

Kamati hiyo ya watu 10, itaongozwa na Profesa Eligius Lyamuya kutoka Chuo Kikuu cha afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (Muhas) tayari imeanza kazi na itatakiwa kuwasilisha ripoti yake kwa waziri kabla ya Mei 13, mwaka huu.

No comments: