Wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa idara ya uandishi wa habari wapigwa msasa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
WANAFUNZI wa chuo kikuu cha Iringa idara ya uandishi wa habari wapigwa msasa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kuwaongezea upeo wa elimu ya uandishi wa habari katika Nyanja mbalimbali za taaluma hiyo.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo afisa wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania Glory Kalinga alisema kuwa lengo la mafunzo hayo kwa ni kuwaongezea uwezo wa kuitambua vizuri taalum hiyo ili wakihitimu masomo wanatakiwa kwenda kutumia taalum hiyo kwa kufuata misingi na kanuni walizopewa wakiwa chuoni.
Alisema kuwa wanafunzi hao wanapaswa kuzijua sheria zilizopo katika sekta ya habari ndio maana wakili yupo kwa ajili ya kutoa elimu ya kisheria na kuendana na sayansi na teknolojia ambayo imekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara.
“Tunatoa elimu hii kwa lengo la kuongeza uelewa na kwa wanafunzi hao wa vyuo vikuu ili wakihitimu masomo yao waendelende wakafanya kazi ya uandishi kwa weredi unaotakiwa kwa kuifanya tansinia hii kuwa imara na yenye wasomi wanaofata maandili,kanuni,sheria na katiba ya nchi” alisema
Aliongeza kuwa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania imekuwa ikitoa mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wa habari mbalimbali kwa lengo la nkumsaidia mwandishi wa habari azitambue haki zake na kujitambua mwenyewe kwenye kazi yake.
Lakini Kalinga aliziomba tasisi na mashirika mengine kuendelea kutoa elimu kwa waandishi wa habari ili kuendelea kuikuza taaluma hiyo ambavyo imekuwa muhimu katika maisha ya wananchi wengi katika nyanja mbalimbali.
Baadhi ya wanafunzi chuo cha Iringa kikuu cha Iringa idara ya uandishi wa habari wamejifunza kwa namna gani wanaweza kupambana na changamoto za tansinia ya habari kutokana naelimu ambayo wamepata kwenye mafunzo hayo ambayo yanafanyika kwa siku tatu katika chuo hicho.
Walisema wanaendelea kujifunza misingi ya wanahabari ili kufanya kazi kwa weredi mkubwa wenye kuzingatia misingi na sheria za taalum hiyo ambayo imekuwa na changamoto nyingi.
No comments:
Post a Comment