Chama cha Mapinduzi (CCM) kimelaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya viongozi wa UWT mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige, baada ya kwenda kuvunja geti na kuingia kwenye makaburi ya familia mahali ambapo amezikwa Kuzula Madoda anayedaiwa kuwa mchumba wake.
Taarifa ya kulaani kitendo hicho imetolewa leo Mei 28, 2021, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, na kusema kuwa CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali, badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.
"Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa Katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM," imeeleza taarifa hiyo.
Haya yote yanajiri baada ya video kusambaa mitandaoni zikimuonesha Mbunge huyo pamoja na watu wengine wakitumia nguvu kushiriki katika mazishi ya mfanyabishara huyo mkoani Arusha
No comments:
Post a Comment