WAKATI kukiwa na kutoelewana baina ya Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez na Msemaji wa Timu hiyo, Haji Manara Mwenyeki wa Klabu hiyo, Murtaza Mangungu ameibuka na kuwataka mashabiki kuwa watulivu.
Mangungu amewataka mashabiki, wapenzi na wanachama wa Timu hiyo ambayo ni Mabingwa mara nne mfululizo wa Ligi Kuu kuwa watulivu na makini kuelekea mchezo wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili Julai 25.
Amesema uongozi wa Simba upo makini na suala la Barbara na Manara na ulishatoa maelekezo ya kutatua mgogoro uliojitokeza na kwamba Simba ni timu inayoendeshwa kiweledi.
” Wote wanaolumbana ni waajiriwa na muajiri yupo, baada ya mashindano tathimini ya mwenendo mzima wa timu na watendaji wake itafanyika lakini kwa sasa kila mmoja wetu azingatie nidhamu, hekima na misingi ya ajira au nafasi yake katika Klabu, nawaomba tuwe watulivu na tuendelee na mikakati ya mchezo ujao,” Amesema Mangungu.
No comments:
Post a Comment