Na.Faustine Gimu Galafoni,Maswa Simiyu.
Baadhi ya Wakulima wa zao la Pamba Wilayani Maswa mkoani Simiyu wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mtandao huu ,akiwemo Diwani wa viti Maalum tarafa ya Sengerema, Maswa Julieth Mongo wamesema hali ya soko ya zao la pamba inaridhisha ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ambapo bei ya zao hilo ni Tsh.1400 hadi 1500 kwa kilo ikivuka lengo kwa bei elekezi ya serikali ambayo ni Tsh.1050.
Wamesema hali ya soko kwa mwaka huu imeleta matumaini makubwa kwao baada ya kukata tamaa kutokana soko ya bei ya zao la pamba kudodorora kwa muda mrefu lakini hali ya soko ya mwaka huu itahamasisha wakulima wengi kujikita katika zao hilo huku pia bei ya mwaka huu ni ya kupewa fedha taslimu ikilinganishwa na kipindi cha nyuma walikuwa wanakopwa pamba mpaka inapita miezi 6 ndipo wanalipwa.
Afisa Kilimo halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Gimu Yohana Mabula amesema Wilaya hiyo imedhamiria kufikisha uzalishaji wa tani laki moja na elfu thelathini[130,000 ]za zao la pamba katika msimu wa 2021/2022 ,lengo ni kuongeza uchumi wa Taifa katika utekelezaji wa kampeni ya uongezaji thamani zao la Pamba nchi nzima ambapo matarajio ni uzalishaji wa tani za pamba milioni moja kote nchini.
Aidha,Afisa kilimo huyo ameainisha upandaji wa vipimo vipya vya zao la pamba kwa msimu wa 2021/22 ni sentimita 60 kati ya mstari na mstari na sentimita 30 kati ya shimo na shimo huku akisisitiza kuwa ifikapo Septemba 15,2021 kila mkulima anatakiwa kuhakikisha masalia yote ya pamba shambani yawe yameshang’olewa na kuchomwa moto.
Hata hivyo leo Julai 30,2021 siku ya Ijumaa , balozi wa Pamba Tanzania Agrey Mwanri anatarajia kufika Wilayani Maswa mkoani Simiyu kuhamasisha kilimo cha pamba .
Ikumbukwe kuwa mkoa wa Simiyu umedhamiria kuongeza tija uzalishaji zao la pamba kutoka kilogram 200 kwa ekari hadi kilogram 800 mpaka 1000 kwa ekari kwa msimu ujao 2021/2022 lengo ni uzalishaji wa tani laki tano
No comments:
Post a Comment