Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akiwa na Naibu wake Dkt Zainab Chaula wakifatilia mada mbalimbali wakati wa Mkutano wa Mapato na matumizi ya wizara hiyo na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Justina Mashiba (kulia),Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo (katikati) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TTCL Bw.Vedastus Mwita (kushoto) wakafatilia mawasilisho mbalimbali wakati wa kikao cha Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile cha kujadili Mapato na matumizi ya wizara yake pamoja na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia kikao cha majadiliano kuhusu Mapato na matumizi ya wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa mapato na matumizi ya wizara na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainab Chaula,akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mapato na matumizi ya wizara hiyo na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Justina Mashiba,akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mapato na matumizi ya wizara hiyo na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu TTCL Bw.Vedastus Mwita ,akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mapato na matumizi ya wizara hiyo na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Kaimu Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo,,akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Mapato na matumizi ya wizara hiyo na taasisi zake kilichofanyika leo Julai 28,2021 jijini Dodoma.
Na Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Dk.Faustine Ndugulile amesema katika kipindi cha Aprili hadi June mwaka huu wamezifungia laini za simu 18,622 ambazo zilikuwa zikitumika kuwatapelia watu mbalimbali huku ikigundua vitambulishi 14,768 vilitumiwa na matapeli kusajili laini hizo.
Akizungumza leo,Julai 28,2021,katika Mkutano wa mapato na matumizi ya Wizara hiyo ,Waziri Ndugulile amesema wamepata taarifa kuna namba ambazo bado zinaendelea kuwatapeli watu hivyo mpaka sasa wamefungia wamezifungia laini za simu 18,622 ambazo zilikuwa zikitumika kuwatapelia watu mbalimbali.
““Tumepata taarifa kuna namba zinaendelea kufanya uhalifu tupo very serious tumefungia line 18,622 kuanzia Aprili mpaka June mwaka huu.Sambamba na hilo namba zote ambazo zilifanya utapeli huo tumezizua vitambulisho vilivyotumika kusajilia laini 14768.
“Ndio maana niwaombe watanzania kuendelea kufanya uhakiki wa laini zetu ili haya yasitokee kwani watu wamesajiliwa na tutawafungia laini kazi hii tunaifanya,Sasa tunaenda kuwatafuta ili tuwafungulie mashtaka tupo Serios katika hili,”amesema.
Aidha,Waziri Ndugulile amewataka watanzania kuendelea kuhakiki namba zao kwani zaidi ya watanzania milioni 10 bado hawajahakiki laini zao.
“TCRA walikuwa wanatoa taarifa ya nusu mwaka kuhusiana na masuala ya uhalifu na kama tunavyokumbuka tulitoa maelekezo ya usajili wa laini kila mtu ahakiki zoezi hili linaenda vizuri lakini bado watanzania wengi zaidi milioni 10 hawahakiki.
“Nitumie fursa hii kuwaomba kuhakiki kwani utaratibu ni rahisi tu.Hili zoezi tupo serious tutaanza kuzizima line zile ambazo hazihakikiwa muhimu sana hauhitaji kusumbuka kwenye simu yako unaweza kufanya uhakiki na utaona line zote zilizosajiliwa,”amesema
Pia,Waziri huyo amesema tangu Wizara imeanza miezi saba iliyopita wameweka mikakati ya ufuatiliaji wa karibu kila baada ya miezi mitatu wana vikao vya kufanya mapitio ya malengo ambayo wamejiwekea, mapato na matumizi lengo ni kujipanga kuifanya kazi vizuri.
“Katika mkutano tumeona mwelekeo wetu ni mzuri kwani taasisi tunazosimamia zimeanza kutekeleza na hali ya utekeloezaji wa malengo ni mzuri na mapato yanaenda vizuri lakini pia tumweza kubana matumizi ili tuendeshe kwa faida,Tumefanya maboresho makubwa TCRA,”Dkt.Ndugulile amesema.
Amesema watendaji ambao watashindwa kufikia malengo katika kila robo watakuwa wakiandikiwa barua za onyo na baada ya muda watachukua hatua kali dhidi yao.
“Hivi ni vikao ni muhimu kila Mtendaji ambaye tumempa kazi ni wajibu ni lazima ahakikishe tunafikia malengo ambayo amepewa na kuelekezwa kufanyanya,”amesema Waziri Ndugulile.
Kwa upande wake,Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Dkt.Zainabu Chaula amesema kikao hicho ni cha kawaida na walikuwa na malengo saba ikiwemo kuhakikisha mawasilino yanafika kila mahali
Amesema wapo na Taasisi sita za Wizara hiyo wanataka kujua wanafanya nini na wamefikia wapi katika malengo na jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali.
“Kimsingi watu wanafanya kazi kubwa na nzuri nikiwa kama Mtendaji mKuu nafurahi tuna mazuri changamoto zipo na tunaendelea kuzitatua Taasisi zangu zimejitahidi kutimiza kwani kwa mwaka huu tumekusanya bilioni 42,”amesema
Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasilino kwa wote (UCSFA) Justina Mashiba amesema wao wameweza kufanya vizuri kwani wameweza kukusanya shilingi bilioni 9 ambapo lengo lililikuwa ni kukusanya bilioni 8 hivyo wamevuka lengo.
“Ninashukuru pia katika hii Quoter ya nne tumeweza kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Studio ya TBC Dodoma na kuweza kuwasha minara ya simu 60 katika maeneo mbalimbali kupitia TTCL,”amesema.
Pia amesema wamepeleaka zabuni ya kupeleka huduma ya mawasilino vijijini ambapo sasa hivi wamejikita kupeleka huduma katika maeneo ya mipakani.
“Tuna mipaka mingi tumetangaza zabuni katika Kata 190 na vilevile tumeweza kupeleka huduma za Mawasilino katika Halmashauri 10,”amesema.
No comments:
Post a Comment