KAMISHNA wa Petroli na Gesi Wizara ya Nishati ,Michael Mjinja,akizindua wa Mwongozo wa usimamizi wa pamoja wa Miundombinu iliyoko chini ya ardhi kwenye Mikuza (wayleave) inayotumiwa na taasisi na Kampuni za huduma mbalimbali kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati.Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam (JTC) Mhandisi Michael Mngodo,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt. James Andilile,hafla iliyofanyika leo Juni 15,2023 jijini Dodoma.
KAMISHNA wa Petroli na Gesi Wizara ya Nishati ,Michael Mjinja,akizungumza wakat wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa usimamizi wa pamoja wa Miundombinu iliyoko chini ya ardhi kwenye Mikuza (wayleave) inayotumiwa na taasisi na Kampuni za huduma mbalimbali kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati hafla iliyofanyika leo Juni 15,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dkt. James Andilile,akizungumza wakat wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa usimamizi wa pamoja wa Miundombinu iliyoko chini ya ardhi kwenye Mikuza (wayleave) inayotumiwa na taasisi na Kampuni za huduma mbalimbali hafla iliyofanyika leo Juni 15,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam (JTC) Mhandisi Michael Mngodo,akitoa taarifa ya kamati tendaji wakat wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa usimamizi wa pamoja wa Miundombinu iliyoko chini ya ardhi kwenye Mikuza (wayleave) inayotumiwa na taasisi na Kampuni za huduma mbalimbali hafla iliyofanyika leo Juni 15,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia Hotuba ya Kamishna wa Petroli na Gesi Wizara ya Nishati ,Michael Mjinja (hayupo pichani) wakat wa hafla ya uzinduzi wa Mwongozo wa usimamizi wa pamoja wa Miundombinu iliyoko chini ya ardhi kwenye Mikuza (wayleave) inayotumiwa na taasisi na Kampuni za huduma mbalimbali hafla iliyofanyika leo Juni 15,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
KAMISHNA wa Petroli na Gesi wizara ya Nishati ,Kamishna Michael Mjinja, amesema ukuaji wa sekta ya gesi asilia nchini umeleta changamoto hasa katika usalama wa miundombinu ya gesi asilia ambayo iko maeneo yanayotumiwa na taasisi zingine katika kufikisha huduma kwa wateja.
Hayo ameyasema leo Juni 15,2023 jijini Dodoma wakati akizindua Mwongozo wa usimamizi wa pamoja wa Miundombinu iliyoko chini ya ardhi kwenye Mikuza (wayleave) inayotumiwa na taasisi na Kampuni za huduma mbalimbali kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati.
Amsema kuwa EWURA kwa kushirikiana na wadau wengine wameandaa Mwongozo wa Usimamizi wa Pamoja wa Miundombinu Iliyoko Chini ya Ardhi Kwenye Mikuza (wayleave) wa Mwaka 2023.
“Mwongozo huo ambao nitauzindua leo kwa dhumuni la kuimarisha usalama wa umma, kuongeza uadilifu na usimamizi makini wa miundombinu iliyopo chini ya ardhi hapa Tanzania Bara”amesema Kamishna Mjinja
Kadhalika, amesema kuwa Mwongozo huo utasaidia katika kuratibu shughuli za ujenzi, uendeshaji, marekebisho na matumizi mengineyo ya mikuza inayotumiwa kwa pamoja na wadau mbalimbali bila kuathiri usalama wa miundombinu, umma na mali zao.
“Hivyo basi, niwatake wamiliki na watumiaji wa mikuza kufuata mwongozo huu pindi wanapofanya shughuli zao”amesema
Ameipongeza EWURA kwa kuratibu zoezi la uandaaji wa mwongozo huo kuanzia mwaka 2019 pamoja na timu za Wataalamu kutoka kwa wamiliki na watumiaji wa Mikuza ( Joint Technical Committee) na Wakuu wa Taasisi ( Joint Steering Commitee) kwa kuridhia mwongozo huu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile,amesema miaka ya hivi karibuni usambazaji wa gesi asilia katika miji ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara umeongezeka.
Amesema ongezeko hili limepelekea shughuli za utandazaji wa miundombinu katika mikuza (wayleaves) inayotumiwa na watoa huduma mbalimbali, yakiwemo mabomba ya usambazaji wa mafuta na maji, miundombinu ya umeme na mawasiliano.
“Shughuli za uchimbaji ili kutandaza miundombinu kwenye mikuza haziepukiki kwani mahitaji ya huduma zinazotolewa na kampuni mbalimbali zinazidi kuongezeka na kufanyika bila ya kuratibiwa (uncoordinated activities); hivyo basi kusababisha uharibifu wa miundombinu iliyofukiwa chini ya ardhi, migogoro na kuhatarisha usalama wa miundombinu hiyo, watu na mali zao”amesema Dkt. Andilile
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam (JTC) Mhandisi Michael Mngodo, alisema kumekua na ongezeko la shughuli zisizoratibiwa kwa pamoja katika utaratibu usio rasmi kwenye miundombinu iliyoko chini ya ardhi hali imayopelekea athari kubwa za kiusalama.
Uharibifu wa mali, mazingira na ajali kwa watu, mfano ni ajali za kupasuliwa kwa mabomba ya gesi asilia, mafuta na maji wakati wa shughuli za ujenzi na maboresho ya miundombinu katika maeneo mbali mbali. Mifano ya ajali kama hizi ipo mingi hasa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayohusisha uchimbaji wa ardhi.
No comments:
Post a Comment